Masharti Ya Jumla Kwa Madereva (itaanza 01.11.2022)
Unaweza kupakua hapa haya Masharti ili uweze kuyapata hata ukiwa nje ya mtandao na kwa matumizi ya baadae.
Masharti haya hutoa vigezo na masharti yanayotumika kuongoza matumizi ya huduma za Bolt.
Ili kutoa Huduma za Usafiri kwa kutumia Jukwaa la Bolt lazima ukubaliane na vigezo na masharti yaliyoainishwa hapa chini.
1. FAFANUZI
1.1. Bolt (pia itatambuliwa kama "sisi" au "yetu") – Bolt Operations OÜ kampuni binafsi iliyosajiliwa chini ya sheria za Jamhuri ya Estonia na namba wa usajili 14532901, iliyosajiliwa Vana-Lõuna tn 15, Tallinn 10134, Jamhuri ya Estonia, pia Kundi la makampuni ya Taxify na washirika wake. Kundi la makampuni ya Taxify itamaanisha ((a) makampuni ambayo Bolt Operations OÜ inadhibiti (mfano matawi/kampuni tanzu ya Bolt Operations OÜ). Washirika wa Taxify itamaanisha wawakilishi, washiriki, mawakala nk walioteuliwa na Bolt Operations OÜ (mfano wakala wa Malipo). Orodha ya kundi la Makampuni ya kundi ya Taxify na washirika wake inapatikana kwenye https://bolt.eu/cities/.
1.2. Huduma za Bolt - huduma zinazotolewa na Bolt, ikijumuisha na utoaji na ukarabati wa Programu ya Bolt, Jukwaa la Bolt, Malipo ya ndani ya Programu, msaada kwa wateja, mawasiliano kati ya Dereva na Abiria na huduma zingine zinazofanana na hizo.
1.3. Programu ya Bolt - programu ya simu janja ya Dereva na Abiria kuomba na kupokea Huduma za Usafiri.
1.4. Jukwaa la Bolt - teknolojia inayounganisha Abiria na Dereva na kuwasaidia kuzunguka miji kwa ufanisi zaidi.
1.5. Abiria - mtu anayeomba Huduma za Usafiri kwa kupitia Jukwaa la Bolt.
1.6. Dereva (pia atatambuliwa nasi kama "wewe") - Mtu anayetoa Huduma za Usafiri kupitia jukwaa la Bolt. Kila Dereva atapata Akaunti binafsi ya Bolt Dereva ili kutumia Programu ya Bolt na jukwaa la Bolt.
1.7. Mkataba – Makubaliano haya kati ya Dereva na Bolt kuhusu matumizi ya Huduma za Bolt yanayojumuisha: 1.7.1. Masharti haya kwa ujumla; 1.7.2. Vigezo maalum vilivyoonyeshwa kwenye Programu ya Bolt, mfano: kuhusu maelezo ya bei au maelezo ya huduma; 1.7.3. Miongozo ya madereva; na 1.7.4. Masharti mengine yaliyotajwa katika makubaliano haya kama yatakavyokuwa yakiboreshwa na kurekebishwa mara kwa mara. Masharti na nyaraka za nyongeza zilizorejewa ama kukubaliwa baina ya Bolt na dereva
1.8. Nauli - Abiria atawajibika kumlipa Dereva nauli kwa utoaji wa Huduma za Usafiri.
1.9. Malipo ya Bolt - Ni ada ambayo Dereva anawajibika kulipa kwa Bolt kwa kutumia Jukwaa la Bolt.
1.10. Malipo ndani ya Programu – kadi, malipo kwa mtoa huduma na malipo mengine na mbinu nyingine za malipo (biashara za Bolt n.k) zinazotumiwa na Abiria kupitia Programu ya Bolt kulipia Huduma za Usafiri.
1.11. Akaunti ya Dereva ya Bolt - upatikanaji wa tovuti iliyo na habari na nyaraka kuhusu matumizi ya Huduma za Bolt wakati wa utoaji wa Huduma za Usafiri, ikiwa ni pamoja na nyaraka za uhasibu. Dereva anaweza kupata Akaunti ya Dereva ya Bolt kwenye https://partners.bolt.eu kwa kuingiza jina la mtumiaji na nenosiri (nywila).
1.12. Huduma za usafiri - huduma za usafiri, Dereva hutoa kwa Abiria ambaye ombi lake la safari Dereva amelikubali kupitia Programu ya Bolt.
1.13. Wakala wa Malipo – Shughuli za Bolt Operations OÜ, yaani, wakala aliye na wajibu wa huduma za kiufundi za kuwezesha utoaji wa huduma za malipo ili kuwezesha malipo na/au ankara kwa niaba ya Bolt Operations OÜ. Wakala wa malipo pia anaweza kujadili malalamiko yoyote na kutatua migogoro yoyote kuhusiana na malipo yaliyofanywa na Bolt Operations OÜ.
2. MUONGOZO WA KUINGIA KATIKA MAKUBALIANO
2.1. Kabla ya kutumia Huduma za Bolt, lazima ujiandikishe kwa kutoa maelezo yaliyotakiwa katika Programu ya usajili kwenye tovuti na kupakia nyaraka muhimu kama zinavyohitajika nasi. Unaweza kujiandikisha kama mtu kisheria au mtu wa asili. Baada ya kukamilisha ombi la kujiandikisha kwenye ya Programu, tutakupa akaunti binafsi itakayopatikana kupitia jina la mtumiaji na nenosiri. Kwa kubofya kitufe cha "Kujiandikisha" kilichopo mwishoni mwa programu ya kujisajili, unathibitisha na kukiri kwamba: kwa mujibu wa matendo ya halali ya kisheria, una haki ya kuingia mkataba na sisi kutumia Jukwaa la Bolt kwa kutoa Huduma ya Usafiri ; umesoma kwa uangalifu, umeelewa kikamilifu na unakubali kufungwa na Masharti haya kwa ujumla, pamoja na majukumu yote yatokanayo na Makubaliano haya; taarifa zote ulizotupatia ni sahihi, yakinifu na kamili; utahakikisha akaunti yako ya dereva ya Bolt na taatifa zako ni sahihi muda wote. Hautoruhusu mtu mwingine kutumia akaunti yako ya dereva wa Bolt wala kuhamisha au kugawa kwa mtu mwingine yeyote; hutotumia Huduma za Bolt kwa madhumuni yasiyoidhinishwa au yasiyo halali na kudhoofisha uendeshaji sahihi ya Huduma za Bolt; wakati wote, utatii kikamilifu sheria na kanuni zote zinazotumika katika nchi unayotoa Huduma za Usafiri, ikiwa ni pamoja na (bila kujikita tu kwenye) sheria zinazosimamia huduma za usafiri wa abiria;
2.2. Unahitajika kutoa taarifa zako za kibenki na huduma za pesa rununu wakati wa kujaza maelezo ya malipo wakati wa usajili. Ikiwa wewe ni mtu kisheria, lazima uweke akaunti ya benki au taarifa za pesa rununu za kampuni. Tunahamisha ada ya malipo ya ndani ya Programu kwenye akaunti ya benki ambayo umetoa. Hatutawajibika kwa shughuli yoyote ya fedha isiyo sahihi ikiwa umetoa taarifa ya benki isiyofaa.
2.3. Baada ya kuwasilisha maombi kwenye Programu ya kujiandikisha, utapokea barua pepe yenye masharti ya ziada ambayo lazima yatimizwe ili utumie Huduma za Bolt. Masharti haya yanaweza kujumuisha kutoa rekodi ya makosa ya jinai, leseni halali ya kuendesha gari, taarifa ya kuridhisha ya kiufundi ya hali ya gari, kukamilika kwa kozi ya mafunzo, kumiliki kifaa cha simu ya mkononi chenye GPS na taarifa nyingine kama ilivyoelezwa kwenye barua pepe itakayotumwa. Kushindwa kuzingatia mahitaji na taratibu zinazotolewa kunaweza kusababisha kusitishwa kwa Mkataba na haki ya kutumia Huduma za Bolt.
2.4. Unakubali kuwa katika miji au nchi maalum Bolt Operations OÜ inaweza kugawa majukumu yetu yoyote yanayotokana na Masharti au Makubaliano kwa ujumla kwa Taxify na makampuni washirika. Hii inajumuisha, pamoja majukumu mengine, kuwapa haki na majukumu juu ya kurekebisha hati zinazohusiana na Programu za kusajili, mafunzo, kukusanya ada za Bolt, kukutumia stahiki zako unazodai, kupatanisha Malipo ya ndani ya Programu, kuidhinisha Programu ya Bolt, nk Maelezo kuhusu kundi la makampuni ya Taxify na washirika wake yanapatikana kupitia https://bolt.eu/cities .
2.5. Kuandikisha akaunti kama mtu kisheria (yaani kampuni). Unachukuliwa kuwa mtu kisheria, kama mpokeaji wa ada ametiwa alama ya mtu kisheria katika maelezo ya malipo (kama inavyoonekana katika Akaunti ya Dereva ya Bolt). Katika hali hiyo, mtu anayeonyeshwa kisheria kuwa mtoa huduma wa Huduma za Usafiri na mmoja wa upande wa Masharti haya, Mkataba na makubaliano yoyote zaidi. Ni mtu wa asili pekee aliyeonyeshwa katika mchakato wa kusajiliwa anaweza kutoa Huduma za Usafiri. Mtu huyo wa asili anaweza kutumia akaunti ya Dereva tu ikiwa amesoma na anakubali kufungwa na Masharti haya na nyaraka nyingine kiujumla ambazo ni sehemu ya Makibaliano haya. MTU KISHERIA KATIKA TAARIFA ZA MALIPO NA MTU WA ASILI ANAETOA HUDUMA ZA USAFIRI CHINI YA AKAUNTI YA BOLT WATABAKI KWA PAMOJA KUWAJIBIKA IWAPO KUTATOKEA UKIUKWAJI WA MASHARTI HAYA YA JUMLA NA TARATIBU YALIYOFANYWA NA DEREVA.
2.6. Kuandikisha Akaunti ya Dereva wa Bolt kama kampuni ya usafirishaji. Baada ya kumaliza makubaliano tofauti, kampuni ya usafirishaji inaweza yenyewe kuandikisha akaunti kwa wafanyakazi wake na / au watoa huduma wake. Katika hali hiyo kampuni ya usafirishaji itahitajika kuhakikisha kwamba inakidhi mahitaji ya Masharti, makubaliano na makubaliano yoyote ya kando kwa ujumla na inakubali kutekeleza shughuli zake kwa kuzingatia masharti na vigezo. Kampuni ya usafirishaji na wafanyakazi wake na/ au watoa huduma wake kwa pamoja watawajibika kisheria kwa ukiukaji wowote utakaofanywa na mfanyakazi na/ au mtoa huduma.
3. HAKI YA KUTUMIA PROGRAMU YA BOLT NA AKAUNTI YA DEREVA YA BOLT
3.1. Leseni ya kutumia Programu ya Bolt na Akaunti ya Dereva ya Bolt. Tunakupa leseni ya kutumia Programu ya Bolt na Akaunti ya Dereva ya Bolt. Leseni haikupi haki ya kutoa leseni ya kando au kuhamisha haki yoyote kwa mtu wa mwingine yeyote asiye sehemu ya makubaliano haya. Mbali na maelezo yaliyotolewa hapo juu na ikiwa kuna makubaliano ya kando, kampuni ya usafirishaji inaweza kuoa leseni za kando za Bolt na akaunit ya dereva ya Bolt kwa wafanyakazi wa kampuni yao.
3.2. Wakati wa kutumia Programu ya Bolt na/ au Akaunti ya Dereva ya Bolt huruhusiwi: kuvunja, kubadilisha kiufundi, au kufanya jaribio la kupata chanzo cha Programu ya Bolt, akaunti ya Dereva ya Bolt au Programu nyingine ya Bolt; kurekebisha Programu ya Bolt au akaunti ya Dereva ya Bolt kwa namna yoyote au njia au kutumia matoleo yaliyobadilishwa ya Programu ya Bolt au akaunti ya Dereva ya Bolt; kusambaza nyaraka zilizo na virusi, faili zilizoharibiwa, au programu nyingine zozote ambazo zinaweza kuharibu au kuathiri vibaya shughuli kwenye Jukwaa la Bolt; kufanya jaribio la upatikanaji usioidhinishwa wa Programu ya Bolt, akaunti ya Dereva ya Bolt au Huduma nyingine za Bolt.
3.3. Leseni iliyotolewa hapa inabatilika moja kwa moja pamoja kufika tamati kwa makubaliano haya. Baada ya kutamatika Makubaliano haya, unatakiwa kusitisha kutumia programu ya Bolt na akaunti ya Dereva ya Bolt mara moja na tuna haki ya kuzuia na kufuta akaunti ya Dereva bila kutoa onyo la awali.
3.4. Kutumia lebo na maandiko ya Bolt. Nyongeza ya hayo, tunaweza kukupa lebo, maandiko, vitambulisho au ishara nyingine ambazo zinaonyesha/zinaashiria alama ya Bolt au vinginevyo zinazo onyesha unatumia Jukwaa la Bolt. Tunakupa leseni isiyo ya kipekee, isiyohamishika ya kutumia nembo hizo na kwa kusudi ya kuonyesha kuwa unatoa Huduma za Usafiri kupitia jukwaa la Bolt tu. Baada ya kusitisha Mkataba lazima uondoe mara moja nembo yoyote inayohusu bidhaa ya Bolt.
3.5. Hakimiliki zote na alama za biashara, ikiwa ni pamoja na msimbo wa chanzo, orodha ya taarifa, nembo na miundo ya ubunifu inayomilikiwa na Bolt na kulindwa na hakimiliki, alama ya biashara na/ au sheria za siri za biashara na masharti ya kimataifa. Kwa kutumia Jukwaa la Bolt au Huduma nyingine za Bolt huna haki yoyote ya umiliki kwa mali yoyote ya ubunifu (akili).
4. KUTOA HUDUMA ZA USAFRI
4.1. Majukumu ya Dereva. Unapaswa kuhakikisha unatoa Huduma za Usafiri kwa mujibu wa Masharti, Mkataba pamoja na sheria na kanuni zinazohusika kwa ujumla pale ambapo unatoa Huduma za Usafiri. Tafadhali kumbuka kuwa utawajibika kwa ukiukwaji wowote wa sheria na kanuni za nci husika ambao unaweza kutokea wakati wa kutoa Huduma za Usafiri.
4.2. Lazima uwe na leseni zote (ikiwa ni pamoja na leseni halali ya dereva), vibali, bima ya gari, bima ya dhima (ikiwa itahitajika), usajili, vyeti na hati nyingine, kofia pamoja na jaketi la usalama pamoja na vifaa vingine vya usalama vinavyohitajika na mamlaka husika katika kutoa Huduma za Usafiri. Ni wajibu wako kuhakikisha uhalali wa nyaraka zote zilizotajwa hapo awali. Bolt ina haki ya kuhitaji uwasilishe ushahidi na kukutaka ukabidhi kwa ajili ya ukaguzi wa leseni, vyeti, vibali, usajili na vyeti.
4.3. Lazima utoe Huduma za Usafiri kwa njia ya kitaaluma kwa kuzingatia maadili ya biashara yanayotumika katika utoaji wa huduma hizo na kujitahidi kutekeleza ombi la Abiria kwa manufaa ya Abiria. Pamoja na mengine, (i)Unapaswa kutumia njia ya gharama nafuu kwa Abiria, isipokuwa abiria akiomba vinginevyo; (ii)Kutosimama au kusitisha safari bila sababu ya msingi; (iii) Hutokua na abiria wengine katika gari isipokuwa Abiria na washirika wake; na (iv) Unapaswa kuzingatia sheria na kanuni zote za barabarani, yaani, huruhusiwi kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu umakini wa kuendesha gari au mtazamo wa hali ya trafiki, ikiwa ni pamoja na kushikilia simu mkononi mwako wakati gari linakwenda.
4.4. Unayo haki ya kipekee ya kuamua wakati unaoweza kutoa Huduma za Usafiri. Utakubali, utakataa au kupuuza Maombi ya Huduma za Usafiri yatakayofanywa na biria na Abiria kwa mapendekezo yako.
4.5. Gharama unazoingia wakati wa kutoa Huduma za Usafiri. Unawajibika na kutunza vifaa vyote na nyenzo muhimu kufanya Huduma za Usafiri kwa gharama zako mwenyewe ikijumuisha simu janja, gari n.k. Pia utawajibika kulipa gharama zote utakazoingia wakati wa kutoa huduma ikiwa ni pamoja na, mafuta, salio la data kwenye, simu janja, bima, ushuru na kodi zote husika, nk. Tafadhali kumbuka kwamba kutumia Programu ya Bolt yanaweza kusababisha matumizi makubwa ya kifurushi cha simu. Hivyo, tunashauri kujiunganisha na kifurushi chenye data kubwa na chenye kuhimili matumizi makubwa ya data.
4.6. Nauli. Una haki ya kutoza nauli kila mara unapokubali kutoa huduma kwa mteja na kukamilisha Huduma ya Usafirishaji kama ilivyoombwa (yaani, Nauli). Nauli imehesabiwa kulingana na bei ya msingi, umbali wa safari husika kama ilivyoelekezwa na kifaa cha GPS na muda wa kusafiri kwajili ya safari hiyo maalum. Bei ya msingi inaweza kubadilika kulingana na hali ya soko la ndani la usafirishaji. Unaweza kufanya mazungumzo juu ya Nauli kwa kututumia ombi ambalo limetia saini kidigitali au kwa mkono. Nyongeza ya hayo, utakuwa na haki ya kumtoza Abiria kiasi cha chini ya kile kilichoonyeshwa na Programu ya Bolt. Hata hivyo, kumtoza Abiria nauli ya ya kiwango kilichoelekezwa na programu ya Bolt haipunguzi gharama ya tozo ya Bolt.
4.7. Tozo ya awali. Abiria anaweza kupewa nafasi ya kutumia chaguo la safari ambayo inaruhusu Abiria kukubaliana na tozo iliyopangwa ya nauli kwa huduma iliyotolewa na wewe (yaani tozo ya awali). Tozo ya awali uainishwa kwa abiria kupitia programu ya kabla ya kufanya ombi la safari, na kwako wakati ombi la safari limekubalika au mwisho wa safari. Nauli iliyohesabiwa kwa mujibu wa kifungu cha 4.6 itatumiwa badala ya tozo ya awali ikiwa Abiria atabadilisha ukomo wa safari wakati wa safari, safari inachukua muda mrefu zaidi kuliko ilivyokadiriwa kutokana na trafiki au mambo mengine, au wakati hali zisizotarajiwa zikaathiri hali ya safari.
4.8. Ikiwa utagundua kuna hitilafu katika hesabu ya Nauli na unataka kufanya masahihisho ya mahesabu ya nauli ,utatakiwa kuwasilisha ombi katika sehemu ya "Marejeo ya Nauli" ya Programu ya Bolt. Kama ombi katika sehemu " Marejeoo ya Nauli" ya Programu ya Bolt halijawasilishwa, Bolt haisahihisha mahesabu hayo ya Nauli wala kukulipa gharama zitokanazo na makosa hayo.
4.9. Bolt inaweza kurekebisha Nauli kwa safari iliyokamilika, ikiwa tutagundua ukiukwaji (kama vile kuchukua njia ndefu au kusimamisha mita ya nauli ya programu ya Bolt baada ya Huduma za Usafiri kuwa zimekamilika) au ikiwa kosa la kiufundi linaloathiri nauli litabainika. Bolt inaweza kupunguza au kufuta bei ya nauli ikiwa tuna sababu ya msingi kuhisi udanganyifu au malalamiko ya Abiria yanaonyesha ukiukwaji uliofanywa na wewe. Bolt itatekeleza haki yake ya kupunguza au kufuta nauli ya safari kwa njia ya kuthibitika na haki.
4.10. Abiria anaweza kulipa ada ya Huduma za Usafiri aidha moja kwa moja au kwa njia ya Malipo ya ndani ya Programu kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 6 cha Masharti haya. Ikiwa Abiria analipa nauli moja kwa moja, ni wajibu wako kukusanya nauli. Ikiwa Abiria atashindwa au anakataa kulipa, Bolt itatuma taarifa ya deni kwa niaba yako. Idhini hiyo inatokana na mamlaka ya uwakala wa malipo uliopewa kwa Bolt na haimaainishi Bolt itakuwa na wajibu wa kulipa malipo ambayo hayajalipwa na Abiria. Ikiwa abiria katika gari hakubali kulipa nauli ya Huduma za Usafiri, nauli italipwa na Abiria ambaye ameamuru utoaji wa Huduma ya Usafiri hiyo. Ikiwa Abiria ataonyesha sababu za msingi za kutokulipa nauli kwa sababu taarifa zako zilizoainishwa katika programu ya Bolt si sahihi, Bolt haitakulipia gharama hizo.
4.11. Risiti. Baada ya utoaji wa huduma za usafiri, Bolt itatengeneza na kupeleka risiti kwa Abiria yenye habari zifuatazo: jina la biashara ya kampuni, mahali pa biashara, jina la kwanza la Dereva, picha ya Dereva, nambari ya leseni ya huduma (ikiwa inafaa), namba ya usajili ya gari, tarehe, wakati, mahali, mwanzo na mwisho wa safari, muda na urefu wa safari, tozo ya awali na nauli iliyolipwa kwa utoaji wa Huduma za Usafiri. Risit ya kila huduma ya usafiri inapatikana kupitia Akaunti ya Dereva wa Bolt.
4.12. Malipo ya kusitisha safari na ada ya kusubiri . Abiria anaweza kusitisha ombi la Huduma za Usafiri ambazo Dereva amekubali kupitia Programu ya Bolt. Dereva ana haki ya kutoza fedha kwa Huduma za Usafiri zilizositishwa (malipo ya kusitisha safari) katika mazingira ambayo abiria amefuta ombi la safari ambalo lilikubaliwa na dereva baada ya muda fulani uliowekwa na Programu ya Bolt.
4.13. Ikiwa, wakati wa utoaji wa Huduma za Usafiri, Abiria au washirika wake wakaharibu gari au vifaa vyake (miongoni mwa hayo, kwa kukwaruza au kutia doa gari au kusababisha harufu mbaya ndani ya gari), utakuwa na haki kuomba Abiria kulipa faini ya hadi (Euro 50) (EUR 50 itabadilishwa kwenda Tanzania shillingi kulingana na bei ya soko kwa siku hiyo). Na kuomba fidia kwa uharibifu wowote unaozidi adhabu. Ikiwa Abiria hakubali kulipa adhabu na / au kulipia gharama za uharibifu, ni lazima utujulishe na tutajaribu kukusanya faini na / au gharama za kufidia uharibifu kwa niaba yako kutoka kwa Abiria. Hata hivyo, hatuchukui dhima yoyote kwa uharibifu wowote unaohusiana na usafi ya gari yaliyosababishwa na Abiria.
4.14. Wajibu wako wa kulipa kodi.Unakubali kwamba unawajibu wa kulipa utokanao na sheria husika zitokanazo na utoaji wa Huduma za Usafiri, ikiwa ni pamoja na (i) Kulipa kodi ya mapato, kodi ya hifadhi ya jamii au kodi nyingine yoyote inayotakiwa; na (ii) Kutimiza majukumu yote ya mwajiriwa na kujisajili kwa kutekelza wajibu wa kulipa kodi kwa ajili ya mahesabu ya kihasibu yatumikayo na nchi Mamlaka za Serikali zinazohusika kama ilivyohitajikana kuelekezwa na sheria husika. Iwapo Mamlaka ya Ushuru itawasilisha maombi ya halali kwetu kutoa taarifa kuhusu shughuli zako, tunataipatia mamlaka hiyo taarifa zako kwa kiasi ambacho kimeruhusiwa na Sheria. Pia, ni wajibu wako kuzingatia kanuni zote za kodi zinazoweza kutumika kuhusiana na utoaji wa Huduma za Usafiri. Hivyo unaridhia kuilipa Bolt ada zote za serikali, madai, malipo, faini au majukumu mengine ya kodi ambayo Bolt itaingia kuhusiana na wajibu utokanao na kanuni husika za kodi ambazo hukuzitekeleza (ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya mapato na ushuru wa mfuko wa hifadhi ya jamii)
4.15. Idhini ya Dereva ya utoaji ankara. Bolt ina haki ya kutoa ankara kwa niaba yako kwa Abiria ili kulipa fidia yoyote ya nauli, adhabu za mkataba au ada nyingine ambazo Bolt hukubaliana nawe. Ankara itatolewa kwako kupitia Akaunti ya Dereva ya Bolt.
5. MALIPO (ADA) YA BOLT
5.1. Ili utumie Huduma za Bolt, unawajibu wa kulipa ada (yaani, malipo ya Bolt). Ada ya Bolt inalipwa kulingana Utaratibu wa Huduma za Usafiri ambao umekamilisha. Kiasi cha ada za Bolt kitawekwa wazi kwako kwa njia ya barua pepe, Programu ya Bolt, akaunti ya Dereva ya Bolt au njia nyingine muhimu. Tafadhali kumbuka kuwa Ada za Bolt zinazotozwa zinaweza kubadilika mara kwa mara, kwa kuzingatia kanuni za uwekaji bei za kamisheni zinazozingatia (i) mizania/ulinganifu wa ugavi na mahitaji ya huduma ya usafiri, (ii) sifa za usafiri ulioagizwa; na (iii) masharti ya kampeni zozote zinazotumika. Ada za Bolt hazitazidi kiwango cha juu zaidi cha Ada za Bolt tulizokutaarifu (‘Kiwango cha Juu Zaidi cha Ada za Bolt’). Hata hivyo, tunaweza kuongeza Kiwango cha Juu Zaidi kinachotumika cha Ada za Bolt wakati wowote kwa kukupatia taarifa kabla.
5.2. Ni Lazima kulipa ada ya Bolt na ada nyingine zozote tunazodai kwako toka mwezi uliopita kuanzia tarehe 15 ya mwezi unaofuata. Utakapochelewa kulipa ada za Bolt, utawajibika ada ya adhabu ya kuchelewesha malipo ya kiasi cha 0.04% (asilimia sifuri kwa asilimia nne) ya kiasi kisicholipwa kwa siku. Pia utawajibika kulipa gharama zetu zote tulizoingia kutokana na shughuli za ukusanyaji madeni.
6. MALIPO YA NDANI YA PROGRAMU (IN-APP PAYMENTS)
6.1. Tunaweza kuwawezesha Abiria kulipia Huduma ya Usafiri kupitia kadi, malipo kwa mtoa huduma, na njia nyinginezo za kulipia (Bolt Biashara n.k) moja kwa moja kwenye Programu ya Bolt (yaani, Malipo ya ndani ya Programu). Unaturuhusu kama mawakala wako wa biashara, kwa dhumuni la kukusanya kwa niaba yako pesa (nauli) au ada nyingine zilizolipwa na Abiria kupitia Ulipaji wa ndani ya programu. Wajibu wowote wa malipo uliofanywa na Abiria kupitia Malipo ya ndani ya Programu utazingatiwa kutimizwa pale malipo yatakapolipwa.
6.2. Hautokataa malipo ya Abiria kupitia malipo ya ndani ya Programu, au kushawishi Abiria dhidi ya matumizi ya Malipo ya ndani ya Programu. Iwapo utakataa Malipo ya ndani ya programu bila sababu ya msingi, tutakuwa na haki ya kukuadhibu kwa faini ya kimkataba ambayo ni kiasi cha Euro 15 kila mara utakapokataa na/ u kuzuia haki yako ya kutumia huduma za Bolt iwapo tabia hii itajirudia (Euro 15 (itabadilishwa kwenda Tanzania shillingi kulingana na bei ya soko kwa siku hiyo).
6.3. Bolt ina haki ya kusambaza msimbo wa ofa kwa abiria kwa maamuzi yetu kwa ajili ya matangazo. Unatakiwa kukubali matumizi ya msimbo wa ofa wakati abiria anatumia msimbo wa programu katika safari kwa kutumia malipo ya kadi. Ofa hazitotumika kwenye safari za kulipwa kwa fedha. Ikiwa matumizi ya msimbo wa ofa yanashukiwa kuwa ni ya udanganyifu, kinyume na sheria, au yametumiwa na Dereva kinyume na vigezo, Masharti na makubaliano yetu kuhusiana na matumizi ya msimbo wa ofa, basi msimbo wa ofa unaweza kufutwa na kiasi kinachobaki hakitalipwa na Bolt kwa dereva.
6.4. Una haki ya kupitia ripoti za malipo ya ndani ya programu kwenye Akaunti ya Dereva ya Bolt au Programu. Ripoti zitaonyesha kiasi cha Malipo ya ndani ya Programu yaliyofanyika wiki iliyopita na pia kiasi ambacho kilishikiliwa kama malipo ya Bolt. Ni Lazima utujulishe kuhusu mazingira yoyote ya muhimu ambayo yanaweza kuathiri majukumu yetu ya kukusanya na kusambaza Nauli ,iliyolipwa kupitia Malipo ya ndani ya programu.
6.5. Hatuwajibiki kukulipa malipo unayoyadai kutoka kwa Abiria ikiwa Malipo ya ndani ya Programu yameshindikana kwa sababu kadi ya malipo ya abiria au malipo mengine yamesitishwa au hayajafanyika kwa sababu nyingine. Katika kesi hiyo tutakusaidia kadai nauli kutoka kwa Abiria na kukupatia muamala wako mara moja pale Abiria anapokuwa amefanya malipo yaliyotakiwa.
6.6. Kabla ya kutoa huduma za usafiri, ni lazima uhakikishe kwamba huduma hiyo imetolewa kwa abiria sahihi au Abiria amethibitisha wazi kwamba anaruhusu abiria wengine wapande kwa kutumia akaunti yake. Ikiwa umekosea katika kumtambua Abiria, na Malipo ya ndani ya programu yamedaiwa kwa mtu, ambaye hajapatiwa au hajaidhinisha Huduma za Usafirishaji kwa abiria wengine, basi tutamlipa mtu huyo malipo yatakayolipwa. Katika kesi hiyo huna haki ya kupokea Nauli kutoka kwetu. Zaidi ya hayo, kwa kila malipo ya ndani ya Programu yaliyofanyika kimakosa, tutakuwa na haki ya kuadhibu kwa faini ya mkataba ya hadi Euro 10 (Euro 10 itabadilishwa kwenda Tanzania shillingi kulingana na bei ya soko kwa siku hiyo).
6.7. Tafadhali kumbuka kwamba tutafanya makato ya nauli zozote zilizolipwa kupitia Malipo ya ndani ya Programu dhidi ya kiasi ambacho unatakiwa kutulipa (yaani, malipo ya Bolt na adhabu za kimkataba). Tuna haki ya kutimiza wajibu wako kifedha Taxify na makampuni washirika, katika hali hiyo tutakua na haki ya kuwasilisha madai dhidi yako. Tunaweza kuondoa dhima zako za kifedha dhidi ya madeni ya kifedha ambayo unayo dhidi yetu.
6.8. Iwapo tutashindwa kulipa stahiki zako kutokana na kurokujumuisha maelezo ya akaunti yako ya benki katika akaunti yako ya Dereva au ikiwa maelezo ya akaunti yako ya benki hayakuandikwa kwa usahihi, basi tutayashikilia malipo hayo kwa siku 180. Ikiwa hutatujulisha juu ya maelezo sahihi ya akaunti ya benki ndani ya siku 180 tangu tarehe ambayo haki ya kudai malipo hayo itaanza, madai yako juu malipo yako yaliyoshikiliwa yatakoma mara moja.
7. MSAADA KWA WATEJA
Tunatoa msaada wa wateja kwa madereva kuhusiana na matumizi ya Huduma za Bolt. Tuna haki ya kuacha kutoa huduma za misaada ya wateja ikiwa umechelewa kufanya malipo yoyote kwa zaidi ya siku 5 (tano) za kalenda.
8. MAKADIRIO NA SHUGHULI
8.1. Ili kuhakikisha tunatoa huduma bora na kuwapa abiria uhakika wa ziada kwa, unatambua kwamba Abiria wanaweza kukupa alama za makadirio na kutoa maoni kuhusu ubora wa Huduma za Usafirishaji ulizotoa. Wastani wa makadirio yako yatahusishwa na akaunti yako ya udereva na itapatikana kwa Abiria kwenye Programu ya Bolt. Iwapo tutagundua kua makadiro aua maoni hayakutolewa kwa nia njema, makadirio au maoni hayo hayatojumuishwa katika mahesabu ya wastani wa makadirio yako ya ubora wa kazi.
8.2. Pamoja na makadirio, tunapima kiwango chako cha shughuli na kukupatia alama ya ufanyaji shughuli (kazi), ambayo inategemea shughuli zako kulingana na kukubali, kutokubali, kutokuitikia na kukamilisha maombi ya Huduma za Usafiri.
8.3. Ili kutoa huduma za kuaminika kwa Abiria, tunaweza kuweka wastani wa makadirio na alama ya chini ya shughuli ambazo Dereva anatakiwa kufikisha na kudumisha. Iwapo, baada ya kuarifiwa nasi, hautoongeza wastani wa makadirio au alama kufikia angalau wastani wa chini katika kipindi kilichoainishwa, akaunti yako ya udereva itasimamishwa moja kwa moja kwa muda au kwa kudumu. Tunaweza kubadili maamuzi ya kusitishwa kwa akaunti yako ikiwa itathibitika kua kwako chini ya wastani kunatokana na sababu zilizo nje ya uwezo wakonau kusimamishwa kwako kumechagizwa na tatizo la kiufundi au makadirio ya uongo.
9. MCHANGANUO WA KIMASOKO NA KAMPENI
9.1. Mchanganuo wa masoko.Tunaweza kukutumia, kupitia Programu ya Bolt, Akaunti ya Dereva ya Bolt,ujumbe mfupi wa simu, barua pepe au njia nyingine, maelezo ya soko, ili kuongeza ufahamu wako kuhusu wakati ambao mahitaji ya Abiria ni ya juu. Mchanganuo huo wa soko ni mapendekezo tu na sio wajibu kwako. Kama ambavyo makadirio ya mchanganuo wa soko yanategemea takwimu zilizopita, hatuwezi kutoa dhamana yoyote kwamba hali halisi ya soko itaendana na makadirio yaliyotolewa katika mchanganuo wa kimasoko.
9.2. Kampeni zinazoahidi mapato ya chini. Tunaweza pia kutoa kampeni, ambazo tutahakikisha mapato ya chini kwa mtoa Huduma za Usafirishaji ndani ya muda ulioainishwa. Ikiwa hautafikia kiwango cha chini kama kilivyoainishwa, tutafidia pengo. Masharti na vigezo maalum vitatumwa kupitia programu ya Bolt, Akaunti ya Dereva ya Bolt, ujumbe mfupi wa simu, barua pepe au njia nyingine. Tunayo haki ya kuamua kama , wakati gani na Dereva yupi tunaweza kutoa kampeni hizo. Ikiwa tuna sababu ya msingi ya kuhisi shughuli yoyote ya kilaghai kwa upande wako, tutashikilia stahiki zako mpaka hapo tuhuma ya ulaghai zitakapokoma na kufutwa.
9.3. Kampeni kwa Abiria. Tunaweza pia kupanga mara kwa mara kampeni mbalimbali kwa Abiria ili kutangaza na kukuza Jukwaa la Bolt. Ikiwa Nauli iliyolipwa na Abiria imepunguzwa kama sehemu ya kampeni hiyo, tutakulipa fidia, kwa thamani ya fedha ya faida inayotolewa kwa Abiria. Tunaweza kufanya makato ya malipo ya masoko dhidi ya ada ya Bolt.
10. UHUSIANO KATI YA WEWE, SISI NA ABIRIA
10.1. Unakiri na kukubali kwamba tunatoa huduma ya jamii ya habari na hatutoi Huduma za Usafiri. Kwa kutumia Jukwaa la Bolt na Huduma za Bolt, tunafanya kazi ya kuunganisha soko la abiria na madereva Abiria na Dereva ili kuwasaidia kuzunguka ndani ya miji kwa ufanisi zaidi. Unakiri kuwa tunatoa Huduma za Usafiri kwa mantiki na misingi ya mkataba wa usafirishaji wa abiria na kwamba tunatoa Huduma za Usafiri kwa kujitegemea au kupitia kampuni kama shughuli za kiuchumi na za kitaaluma. 10.2. Unakiri kuwa hakuna makubaliano ya ajira wala uhusiano wa ajira umeingiwa au utaanzishwa kati yako na sisi. Pia unakubali kuwa hakuna ubia au ushirikiano uliopo kati yako na sisi. Hautofanya kazi kama mfanyakazi, wakala au mwakilishi wetu au kuingia mkataba wowote kwa niaba yetu. Ikiwa ni kwa sababu ya matakwa ya lazima kisheria au vinginevyo, utachukuliwa kama mfanyakazi wetu, unakubali kutokua na madai yoyote dhidi yetu ambayo yatatokana na mahusiano hayo ya ajira.
10.3. Hautohamisha haki na majukumu yako yanayotokana na Masharti kwa ujumla pamoja na makubaliano haya kwa mtu yeyote asiye sehemu ya makubaliano haya.
11. UHIFADHI WA TAARIFA ZAKO BINAFSI
11.1. Taarifa zako binafsi zitahifadhiwa kwa mujibu wa Taratibu za Faragha, zinazopatikana katika https://bolt.eu/sw/legal/tz/privacy-for-drivers/
12. DHIMA
12.1. Jukwaa la Bolt hutolewa kwa "kama lilivyo" na "kama inavyopatikana" kimsingi. Hatufanyi uwakilishi na tunathibitisha na kuhakikisha ya kwamba upatikanaji wa Jukwaa la Bolt hautaingiliwa au kupata hitilafu. Kwakua matumizi ya Jukwaa la Bolt ya kuomba huduma za usafiri yanategemea tabia ya Abiria, hatukuhakikishi kwamba matumizi yako ya Jukwaa la Bolt yatasababisha kupata maombi yoyote ya Huduma za Usafiri.
12.2. Kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria husika, sisi, wala wawakilishi wa Bolt, wakurugenzi na wafanyakazi hatutawajibika katika hasara au uharibifu wowote utakaojitokeza sababu ya kutumia Huduma za Bolt, ikiwa ni pamoja na; Uharibifu wa namna yoyote wa mali au hasara kifedha; upotevu wa faida au akiba ya kutarajia upotevu wa biashara; upotevu wa biashara, kandarasi, mikataba, mawasiliano, nia njema, sifa na hasara yoyote ambayo itokanayo na kuingiliwa kwa biashara; upotevu au ukosewaji wa taarifa na; aina yoyote ya hasara au uharibifu.
12.3. Dhima yetu ya kifedha itokanayo na ukiukwaji wa Masharti na Makubaliano haya hautazidi Euro 500 (Euro 500 itabadilishwa kwenda Tanzania shillingi kulingana na bei ya soko kwa siku hiyo). Utakuwa na haki ya kudai fidia tu ikiwa tumevunja kwa makusudi Masharti au Makubaliano haya.
12.4. Hatutawajibika kwa matendo au kutokutenda kwa abiria au washirika wake na hautowajibika kwa hasara au uharibifu ambao unaweza kujitokeza kwako na kwa gari yako kama matokeo ya vitendo au kutokutenda kwa abiria na washirika wake.
12.5. Utawajibika kwa uvunjaji wa masharti kwa ujumla na makubaliano au sheria na kanuni zozote husika na utatakiwa kuacha na kutatua uathari za ukiukwaji huo baada ya kupokea madai kutoka kwetu an mamlaka yoyote ya nchi. Utatulipa fidia kwa upotevu au uharibifu wowote wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja, upotevu wa faida, gharama, faini ambayo itatokana na ukiukwaji wako wa Masharti, makubaliano kwa ujumla na sheria na kanuni. Kama abiria ataleta malalamiko dhidi yetu kutokana na huduma za safari ulizotoa wewe, basi utawajibika kutulipa fidia za madai hayo yote ndani ya siku saba (7) baada ya kupokea taarifa ya madai hayo kutoka kwetu. Iwapo tuna haki ya kufungua madai yoyote dhidi yako, basi utawajibika kutulipa gharama zozote za kisheria zitakazotokana na tathmini ya uharibifu na uwasilishwaji wa madai yanayohusiana na fidia kwa uharibifu huo.
13. MASHARTI NA UKOMO
13.1. Masharti yaliyoelezwa wazi katika Makubaliano haya kwa ujumla, yataingizwa katika uwasilishaji wa maombi ya kujisajili. Makubaliano haya na vipengele vingine yataanza baada ya nyaraka maalum na ujumbe umewekwa wazi kwako na umeanza au umeendelea kutoa huduma za usafirishaji katika jukwaa la Bolt.
13.2. Unaweza kusitisha Makubaliano wakati wowote kwa kuitaarifu BOLT siku saba kabla kusitisha makubaliano, baada ya hapo haki yako ya kutumia Jukwaa la Bolt na Huduma za Bolt itakoma. Bolt inaweza kusitisha Makubaliano wakati wowote na kwa sababu yoyote ndani ya mamlaka yetu kuktaarifu siku tatu kabla ya usitishaji huo.
13.3. Bolt ina haki ya kusitisha Makubaliano haya na kuzuia ufikiaji wako wa Jukwaa la Bolt bila kutoa taarifa yoyote ya awali ikiwa unakiuka masharti na Makubaliano haya, sheria yoyote au kanuni, yenye kuathiri bidhaa, sifa au hadhi ya biashara ya Bolt kwa mamlaka yetu. Katika masuala yaliyotajwa hapo juu tunaweza, kama ilivyo ndani ya uwezo wetu, kukukataza kusajili akaunti mpya ya dereva.
13.4. Tunaweza pia, kuzuia uwezo wako wa kulifikia Jukwaa la Bolt na Akaunti ya Dereva ya Bolt kwa kipindi chote cha uchunguzi, ikiwa tuna sababu yakinifu za kuhisi ukiukwaji wa Makubaliano au shughuli za udanganyifu kutoka kwako. Kizuizi kitaondolewa mara baada ya uchunguzi kuthibitisha tuhuma hizo si za kweli.
13.5. Tuna lengo la kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa Abiria wote, hivyo tunafuatilia shughuli za Dereva kwenye Jukwaa la Bolt. Iwapo utashindwa kufikia vigezo vya chini vya kutoa huduma, kama kupata alama ndogo ya makadirio ya utoaji wa huduma, tuna haki ya kusitisha Makubaliano mara moja bila kutoa taarifa yoyote.
14. MABORESHO
14.1. Mabadiliko yoyote ya Makubaliano yataanza kutumika baada ya kuwezeshwa kupatikana kwa njia ya barua pepe, Programu ya Bolt au Akaunti ya Dereva ya Bolt na kama umeendelea kutoa Huduma za Usafiri.
14.2. Ili kurekebisha Masharti haya kwa ujumla, tutaweka toleo jipya kwenye tovuti (https://bolt.eu/legal/) na kutoa taarifa ya awali ya angalau siku 14 (kumi na nne) kabla ya mabadiliko hayo hayajafanyika. Ikiwa utaendelea kutumia Huduma za Bolt, utakua umekubali masharti kama yalivyorekebishwa.
15. SHERIA INAYOHUSIKA NA MAMLAKA YA KIMAHAKAMA
15.1. Masharti na makubaliano kwa ujumla yatasimamiwa, kutafsiriwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Estonia. Ikiwa mgogoro utokanao na Masharti na Makubaliano haya, umeshindwa kutatuliwa kwa mazungumzo na mapatano, basi Mgogoro huo utatatuliwa kwa Mujibu wa Mahakama ya Harju Mkuu hauwezi kutatuliwa kwa mazungumzo, basi mgogoro utatatuliwa katika Mahakama ya Kata ya Harju.
16. TAARIFA
16.1. Unawajibu wa kutufahamisha mara moja juu ya mabadiliko ya taarifa zako ya mawasiliano. 16.2. Taarifa yoyote inayohitajika kwa mujibu masharti na makubaliano haya kwa jumla itatolewa kwa ukamilifu ikiwa: (i) Hutolewa binafsi, (ii) itatumwa kwa kutumia mjumbe kuwepo na ushahidi wa utumaji, (iii) itatumwa katika anuani iliyosajiliwa, (iv) itatumwa kwa barua pepe au (v) itawekwa wazi kupitia programu ya Bolt au Akaunti ya Dereva ya Bolt. Taarifa yoyote iliyotumwa kwa mujibu wa kifungu hiki itachukuliwa kuwa imepokelewa: (i) Ikiwa itafanywa binafsi, wakati wa kufikishwa kwa upande mwingine; (ii) Ikiwa itatumwa kwa kutumia mjumbe kuwepo na ushahidi wa utumaji wa mjumbe ikiwepo tarehe katika bahasha yenye taarifa iliyofikishwa kwa upande mwingine, (iii) ikiwa itatumwa katika anuani iliyosajiliwa, katika siku ya kumi baada ya kuikabidhi barua yenye taarifa hii posta kwa ajili ya kufikishwa kwa upande wa pili, (iv) ikiwa itawekwa wazi kupitia programu ya Bolt au Akaunti ya Dereva ya Bolt, au (v) ikiwa imetumwa kwa barua pepe au hutolewa na barua pepe, kwa tarehe iliyoelezwa na barua pepe kama siku ambayo bahasha iliyo na taarifa ilitolewa kwa chama; katika siku ambayo upande wa mpokea barua pepe utathibitisha kupokea barua pepe au siku ya pili baada ya kutuma barua pepe hiyo iliyoandaliwa na mtumaji bila ya kupokea taarifa barua pepe hiyo kua na hitilafu (kutaharifiwa kwamba barua pepe haikumfikia mhusika) na ametuma barua pepe tena katika siku iliyofuata kwa mujibu wa kalenda na haijapokelewa na taarifa ya hitilafu imetumwa kama hapo awali .
17. MASHARTI YA MWISHO
Kama kifungu chochote cha Makubaliano haya kwa ujumla hakitekelezeki, pande za makubaliano haya zitabidili kifungu hicho ambacho hakietekelezeki kwa kifungu chenye maana ya karibu na kifungu kilichoathirika kwa kuzingatia athari zake kiuchumi.