Vigezo Na Masharti Kwa Abiria

Vigezo na masharti haya yamewekwa ili kuonyesha taratibu na kanuni zitakazotumika kuongoza na kuendesha matumizi ya teknolojia ya Programu ya Bolt inayounganisha abiria na madereva ili kuwasaidia kuzunguka ndani ya miji kwa ufanisi zaidi

Neno "sisi" linamaanisha mmiliki wa Programu ya Bolt, Bolt Operations OÜ, kampuni binafsi, iliyoanzishwa katika Jamhuri ya Estonia ( Yenye Namba ya Usajili wa Kampuni 14532901), ambayo makazi/ofisi yake ya biashara iko Vana-Lõuna tn 39 / 1, Tallinn 10134, pia kwa Makampuni ya Bolt na washirika wake (matawi ya ndani, wawakilishi, washirika, mawakala nk). Orodha ya Makampuni ya Bolt na washirika wake inapatikana https://bolt.eu/cities/.

Ili kutumia programu ya Bolt, ni lazima kukubaliana na Vigezo na masharti haya kama vilivyoainishwa hapa chini:

1. KUTUMIA PROGRAMU YA BOLT

1.1. Bolt hutoa ya huduma ya habari za jamii na haitoi huduma za usafiri. Huduma za usafiri hutolewa na madereva chini ya mkataba (pamoja na wewe) kwa ajili ya kumsafirisha abiria. Madereva hutoa huduma za usafiri kwa misingi ya kujitegemea (aidha kama mtu binafisi au kupitia kampuni) kama watoa huduma kwa sababu za kiuchumi na kama wataalamu. Migogoro inayotokana na haki za wateja au watumiaji, wajibu kisheria au sheria husika zinazohusaiana na kutoa huduma za usafiri itatuliwa baina ya abiria na madereva. Taarifa kuhusu madereva na huduma zao za usafiri zinapatikana katika Programu ya Bolt na risiti za safari zinatumwa kwa barua pepe iliyoorodheshwa katika wasifu wa abiria.

1.2. Wakati wa kutumia Programu ya Bolt, unaweza kuchagua kumlipa dereva kwa huduma ya usafiri au kutumia huduma za malipo ndani ya programu ya Bolt. Malipo ya uendeshaji wa Biashara ya Bolt hutumiwa kwa makubaliano tofauti kwa ajili ya safari za Biashara. Malipo yatajumuisha kodi zinazoelekezwa kisheria. Malipo yanaweza kujumuisha ada nyingine husika, pesa, na / au ada za ziada ikiwa ni pamoja na ada ya uhifadhi nafasi, ada za manispaa, malipo ya uwanja wa ndege au kutathmini malipo ya mgawanyo.

1.3. Wakati wa uwekaji wa Programu ya Bolt, nambari ya simu ya abiria itaunganishwa na akaunti ya mtumiaji wa Bolt na kuongezwa kwenye orodha yetu ya kutunzia taarifa. Ikiwa hutumii namba yako ya simu tena, lazima utujulishe Bolt ndani ya siku 7 ili tuweze kufuta taarifa zako za akaunti. Ikiwa haujatujulisha kuhusu mabadiliko yoyote kwa namba yako ya simu, mtoa huduma wako wa mtandao wa simu anaweza kupitisha namba hiyo ya simu kwa mtu mwingine na wakati mtu huyo anatumia programu ya Bolt, anaweza kuona taarifa zako.

1.4. Wakati wa kutumia huduma ya Boda Boda za Bolt, tambua, kuvaa kofia na jaketi la usalama ni matakwa ya sheria na una wajibu wa kudai vifaa hivi kutoka kwa dereva kabla ya kuanza safari, pia utatakiwa kuvaa vifaa vya usalama kwa muda wote wa safari na kurudisha vifaa hivyo kwa dereva baada ya kukamilika safari

2. KANUNI ZA MATANGAZO

2.1. Bolt inaweza kukutumia nambari za matangazo kwa misingi ya kujitangaza. Ofa ya msimbo wa matangazo inaweza kutumika kulipia safari na huduma zinazotolewa kwa watu wasio sehemu ya makubaliano haya kwa mujibu wa vigezo na masharti ya ziada yatakayoainishwa kwa minajiri ya matangazo.. Tarehe ya ukomo wa msimbo wa matangazo utaonekana kwenye akaunti yako ya programu ya Bolt mara baada ya kutumia msimbo huo.

2.2. Kama gharama ya safari yako inazidi kiasi kilichotolewa kama sehemu ya msimbo wa matangazo, gharama baki salio itakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mifumo/nyenzo zako za malipo zilizoainishwa katika ya akaunti yako ya Bolt. Vilevile, msimbo wa matangazo ya ofa utatumika tu kwa ajili ya safari moja, hauwezi kutumika kwa safari nyingine na utafutwa baada yta kukoma kwa safari. Msimboi mmoja tu waz\ afa unaweza tumika kwa ajili ya safari moja.

2.3. Bolt ina haki ya kusitisha msimbo wa promosheni wakati wowote kwa sababu yoyote. Hii inajumuisha, iwapo Bolt itaona kuwa misimbo inatumika katika namna isiyo ya halali au ya ulaghai, kama zile zilzotolewa kwa makosa, na zile ambazo zimefika tamati.

3.MALIPO YA NDANI YA PROGRAMU YA BOLT (IN-APP PAYMENT)

3.1. Unaweza kulipia huduma za usafiri kwa kadi, simu ya mkononi na mbinu nyingine za malipo (kama: kupitia Biashara za Bolt nk), ambazo zinahitaji kufunguliwa kabla ya kuzitumia kupitia Programu ya Bolt. Kwa kutoa huduma ya Malipo kupitia malippo ya ndani ya programu ya Bolt, Bolt huwa kama wakala wa watoa huduma za usafiri. Wajibu wako kwa mtoa huduma ya usafiri utatimizwa wakati utaratibu wa kulipa ukishatolewa kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti ya benki ya Bolt. Wewe, kama abiria unawajibika kuhakikisha kuwa malipo yanafanyika na kuhakikisha una fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya malipo haya.

3.2. Wakati wa kufanya malipo ndani ya programu ya Malipo ya Bolt, Bolt itapokea malipo yako na kuyatuma kwa dereva. Bolt inaweza kuomba taarifa za ziadi kutoka kwako ili kuthibitisha njia yako ya malipo.

3.3. Wakati wa kufanya malipo ndani ya programu ya Malipo ya Bolt kwa ajili ya huduma za usafiri, Bolt haitawajibika kwa gharama za malipo ya asiye sehemu ya makubaliano haya (mf. mitandao ya simu, ada za benki nk). Watoa huduma hawa wanaweza kukutoza ada za ziada wakati wa kufanya malipo ya ndani ya programu ya Malipo. Bolt haitawajibika kwa ada yoyote na inakataa dhima zote katika suala hili. Njia yako ya malipo inaweza kuhusishwa na masharti na vigezo vya ziada viliyowekwa na mtoa huduma wa malipo; rejea soma vigezo na masharti haya kabla ya kutumia njia yako ya malipo.

3.4. Bolt itawajibika katika ufanyaji kazi wa programu ya ndani ya malipo ya Bolt na kutoa msaada katika kutatua matatizo. Azimio la migogoro inayohusiana na programu ya ndani ya malipo ya Bolt hufanyika kupitia kwetu. Kwa msaada wa huduma za malipo wasiliana na: info@bolt.eu.

4. KUAGIZA NA KUFUTA HUDUMA ZA USAFIRI

4.1. Ukiagiza huduma ya usafiri na dereva akakubali kutoa huduma hiyo, itachukuliwa kama ombi la huduma limefanyika.

4.2. Mara dereva atakapothibitisha kwamba kamaliza safari yako, utaingia maqkubaliano ya kando na dereva kwa ajili ya utoaji wa huduma za usafiri kwa masharti kama vile mtakavyokubaliana na dereva. Bolt haitoi huduma za usafiri na haitokuwa sehemu ya makubaliano yako na dereva husika.

4.3. Kusitisha matumizi ya huduma ya usafiri iliyoagizwa itatambulika pale ambapo dereva amejibu ombi lako la safari na baadae kukataa au na wewe kusitisha au kukataa ombi hilo la huduma ya usafiri. Wakati ombi la huduma ya usafiri limefutwa baada ya muda fulani huhitajika kulipa ada ya kufuta ombi hilo.

4.4. Iwapo utasitisha ombi la huduma za usafiri mara nyingi mfululizo ndani ya saa 24 tunaweza kuzuia akaunti yako kwa muda mfupi kama onyo. Baada ya maonyo mengi, tunaweza kusimamisha akaunti yako kwa muda mrefu (mfano: miezi 6). Baada ya kipindi hicho unaweza kuomba ili akaunti yako iachiwe huru na maombi yako yatarejewa na Bolt.

4.5. Dereva atakapomfahamisha abiria kua amefika eneo la lumchukulia bairia na abiria au washirika wake wakashindwa kufika katika muda uliopangwa katika programu ya Bolt, ombi litasitishwa. Wakati mwingine dereva anaweza kuamua kufuta ombi lako, tafadhali tambua kuwa Bolt haitawajibika katika hali kama hiyo.

4.6. Mara dereva anapowasili na kukutumia taarifa kwamba amewasili, Programu ya Bolt inaweza kuanza kutoza nauli kwa wakati wote wa kusubiri kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa katika Programu ya Bolt.

4.7. Iwapo umefanya maombi ya huduma za usafiri kwa kutumia Programu ya Bolt na kusababisha uharibifu wa gari na vifaa vyake (miongoni mwa hayo kukwaruza au kusababisha doa kwenye gari au kusababisha gari kuharibika), dereva atakuwa na haki ya kukudai fidia ya hadi EURO 50 ili kufidia uharibifu huo, Bolt inaweza kudai kwa niaba ya mtoa huduma wa usafiri.

5. LESENI YA KUTUMIA PROGRAMU YA BOLT

5.1. Maadamu unakubali kufuata vigezo na masharti haya, tunakubali kukupa huduma bila gharama za mrahaba, unayoweza kutamatisha, ambayo unaweza kuifikia na kutumia Programu ya Bolt kwa mujibu wa Kanuni na Masharti haya.taarifa ya kanuni za Faragha na sheria husika za kuhifadhi Programu. Hutaruhusiwa kuhamisha au au kukodisha haki ya kutumia Programu ya Bolt, na ikitokea umefanya hivyo haki yako ya kutumia programu ya Bolt itasitishwa.

6. DHIMA

6.1. Kwakua Programu ya Bolt ni huduma ya habari za jamii (njia ya mawasiliano) kati ya abiria na madereva, hatuwezi kuthibitisha au kuwajibika kwa lolote linalohusiana na kasoro au ubora katika utoaji wa huduma za usafiri. Katika matumizi ya Programu ya Bolt ya kuomba huduma za usafiri inategemea tabia ya madereva, Bolt haithibitishi kwamba daima utapata huduma zinazopatikana kwenye utoaji wa huduma za usafiri.

6.2. Programu ya Bolt haitoi wala sio dalali wa huduma za usafiri kwa abiria. Pia sio wakala wa huduma za usafiri kwa ajili ya kuwatafutia abiria watoa huduma za usafiri. Programu ya Bolt ni njia ya kupangilia utoaji wa huduma za usafiri.

6.3. Haki ya mtumiaji huduma kulipwa rejesho haitumiki katika Amri ya Programu ya Bolt. Kuomba marejesho kutokana huduma za usafiri hakukuondoa katika makubaliano haya wakati unapofanya maombi ya huduma za usafiri.

6.4. Programu ya Bolt kimsingi hutolewa "kama ilivyo" na "kama inavyopatikana". Bolt haiwakilishi, haihakikishi wala kuthibitisha kwamba hakutakua hitilafu ya kimtandao katika upatikanaji wa Programu ya Bolt. Iwapo kuna makosa yoyote katika Programu, tutajitahidi kuyasahihisha haraka iwezekanavyo, lakini kumbuka, utendaji wa Programu unaweza kuzuiwa kutokana na makosa ya kiufundi na hatuwezi kukuhakikisha kwamba Programu itafanya kazi wakati wote, kwa mfano inapotokea dharura ya umma inaweza kusababisha usumbufu wa huduma.

6.5. Bolt, wawakilishi, wakurugenzi na wafanyakazi wake hawatawajibika kwa hasara au uharibifu wowote utakaojitokeza kama matokeo ya kutumia au kuitegemea Programu ya Bolt, safari iliyoanzishwa kwa njia ya programu ya Bolt, ikiwa ni pamoja na:uharibifu wowote ikiwemo uharibifu wa mali au upotevu wa fedha; upotevu wa faida; upotevu wa biashara, mikataba, mawasiliano, sifa na hasara yoyote ambayo inaweza kutokea kutokana na kusumbuliwa kwa biashara; kupoteza usahihi wa taarifa; na aina yoyote ya upotevu au uharibifu.

6.6. Dhima ya kifedha ya Bolt juu ya uvunjaji wa mkataba itakuwa mpaka kiasi cha Euro 500. Utakuwa na haki ya kudai fidia kama Bolt imevunja mkataba kwa makusudi. Bolt haitawajibika kwa vitendo vya dereva na hadha na uharibifu vitakayosababisha kwa abiria.

6.7. Unakubali kufidia na kutokuiwajibisha Bolt, makampuni washrika, pamoja na wawakilishi, wafanyakazi na wakurugenzi wake dhidi ya madai au hasara yoyote (ikiwa ni pamoja na dhima, uharibifu, na gharama na matumizi ya namna yoyote) ambayo yatasababishwa na matumizi yako ya Programu ya Bolt (ikiwa ni pamoja na safari unafanya kupitia matumizi yako ya Programu ya Bolt).

6.8. Bolt inaweza kusitisha matumizi yako ya Programu ya Bolt mara moja kama utakiuka vigezo na Masharti haya au kama tunadhani ni muhimu kusitisha matumizi yako kwa ajili ya kulinda uadilifu wetu au usalama wa madereva.

7. MATUMIZI MAZURI YA PROGRAMU YA BOLT

7.1. Kwakua Bolt si mtoa huduma au dalali wa huduma za usafiri, masuala yote ya kasoro na ubora wa huduma za usafiri yatatatuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utoaji huduma wa usafiri au mamlaka ya umma husika.

7.2. Tutakuomba kujaza fomu ya maoni katika Programu ya Bolt. Hii inatuwezesha kutoa mapendekezo kwa madereva kwa ajili ya kuboresha ubora huduma za usafiri.

7.3. Tunatarajia utatumia Programu ya Bolt kwa nia njema na utawaheshimu madereva wanaotoa huduma za usafiri kupitia Programu ya Bolt. Bolt ina haki ya kufunga akaunti yako ikiwa umekiuka masharti yaliyowekwa katika vigezo na Masharti, au ikiwa shughuli zako ni za kushhukiwa, yaani kushikia malipo ya utoaji wa huduma za usafiri, ulaghai, kutokuheshimu madereva, nk. Katika matukio haya, akaunti yako ya Programu ya Bolt inaweza kufutwa bila ya taarifa yoyote.

7.4. Bolt itajitahidi kuhakikisha madereva waadilifu na weledi na wenye kuheshimu kazi yao pamoja na abiria pekee ndio wanaotumia programu ya Bolt. Hata hivyo, hatuko katika nafasi ya kukuhakikishia kwamba kila mtoa huduma za usafiri, zilizoko kwenye Programu yetu ya Bolt, atakua amekidhi vigezo vilivyotajwa hapo juu wakati wote. Iwapo, utakutana na huduma duni za usafiri, tafadhali wajulishe kampuni husika na utoaji huduma, mamlaka ya usimamizi au msaada wetu wa wateja.

8. MABORESHO YA VIGEZO NA MASHARTI

8.1. Kama marekebisho makubwa yatafanywa katika vigezo na Masharti, utaarifiwa kwa barua pepe au kupitia Programu ya Bolt. Iwapo utaendelea kutumia Programu ya Bolt baada ya mabadiliko hayo, utakua umekubaliana na marekebisho hayo.

9. MASHARTI YA MWISHO

Vigezo na Masharti haya vitaongozwa na, kuainishwa, kutafsiriwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Estonia. Iwapo kutakua na mgogoro unaotokana na Vigezo na Masharti haya hauwezi kutatuliwa kwa maridhiano, mgogoro huo utatatuliwa katika Mahakama ya kitongoji cha Harju huko Tallinn, Estonia. Iwapo, kifungu chochote cha masharti haya hakiwezi kutekelezeka, pande za makubaliano haya zitabadili kifungu hicho kwa na kifungu kinachotafsirika kwa kifungu chaenye maana kairbu sawa na kile cha awali na athari yenye kufanana kiuchumi.

Tarehe ya kuanza kutumika kwa Masharti: 21.03.2019.

Scan to download

Almost there!

Scan the QR code with your phone’s camera to download the app.