Sera Ya Faragha Kwa Dereva
Bolt Operations OÜ (Namba ya Usajili wa Kampuni 14532901) yenye ofisi zake Vana-Lõuna tn 15, Tallinn 10134, Estonia, ni muongozaji wa taarifa binafsi za abiria na amechagua Afisa Ulinzi wa Taarifa (privacy@bolt.eu).
Neno "sisi" linamaanisha mmiliki wa Programu ya Bolt, Bolt Operations OÜ, kampuni binafsi, iliyoanzishwa katika nchi ya Jamuhuri ya Estonia.
1. Mchakato wa taarifa binafsi
- Jina, barua pepe, nambari ya simu, anuani ya makazi.
- Eneo la ki-jiografia la dereva na njia za kuendesha gari.
- Taarifa kuhusu magari (ikiwa ni pamoja na nambari ya usajili).
- Ufanisi wa dereva na tathimini ya malipo.
- Leseni ya dereva, picha, nyaraka za taaluma na hati za utambulisho.
- Taarifa kuhusu makosa ya jinai. Takwimu za kifedha za kutoa huduma za usafiri hazipatikani kama taarifa binafsi, kwa sababu madereva hutoa huduma kama shughuli za kiuchumi na za kitaaluma.
2. Malengo ya uhifadhi wa taarifa
- Tunakusanya na kutunza taarifa binafsi kwa lengo la kuunganisha abiria na madereva ili kuwasaidia kuzunguka ndani ya miji kwa ufanisi zaidi.
- Njia za uendeshaji wa eneo la ki-jiografia zinatatuliwa ili kuchambua eneo la kijiografia na kutoa mapendekezo kwa madereva. Ikiwa hutaki kuonesha eneo lako la kijiografia kwa abiria, ni lazima ufunge programu ya Bolt au uonyeshe kwenye programu ya Bolt kwamba uko nje ya mtandao na kwa muda huo hutoi huduma za usafiri.
- Leseni ya dereva, taaluma, nyaraka za utambulisho na uhalifu wa makosa ya jinai zitahifadhiwa ili kuzingatia mahitaji ya kisheria na uwezekano wa kujiboresha kiajira kama dereva.
- Programu ya Bolt itaonyesha picha ya dereva, maelezo na jina la gari kwa abiria ili kutambua dereva na gari.
- Utapokea muhtasari kutoka Wavuti ya Dereva ya Bolt, ambayo itajumuisha ufanisi na tathmini yako kama dereva. Muhtasari na tathmini kuhusu dereva ni muhimu ili kutoa huduma za kuaminika kwa abiria.
- Tunakusanya na kutumia taarifa kuhusu ushiriki wa madereva na mwingiliano sokoni, na ukadiriaji wao (pamoja na Kiwango cha ufaulu wa dereva) ili kuhimiza usalama wa mtumiaji, kuhakikisha kuwa unatii Sheria na Masharti ya Dereva, na tuhakikishe tunatoa huduma bora na ya kufurahisha kwa kila mtu. Ambapo Kiwango cha ufaulu wa dereva kinashuka chini ya kiwango maalum, tunaweza kukupa taarifa au kukuomba, kwa mfano, chunguza mwongozo zaidi. Ikiwa alama yako itaendelea kushuka, utasimamishwa kwa muda kufikia jukwaa la Bolt. Unaweza kukata rufaa kwa uamuzi wowote wa kusimamishwa akaunti yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kusimamisha akaunti yako, tafadhali tazama Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu Kiwango cha ufaulu wa dereva hapa ↗.
3. Misingi ya kisheia
- Taarifa binafsi zinahifadhiwa kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini na dereva. Uhifadhi wa utambulisho wa dereva na taarifa ya eneo la ki-jiografia ni mahitaji ya lazima kwa matumizi ya huduma za Bolt.
- Taarifa binafsi zinaweza kutumiwa chini ya maslahi ya halali katika kuchunguza na kutambua malipo ya udanganyifu.
- Taarifa kuhusu uhalifu na makosa ya jinai hutumiwa kufuatana na mujibu wa sheria.
4. Wapokeaji wa taarifa
- Taarifa zako binafsi zitatolewa kwa abiria, pale tu ombi lake litakapokubaliwa na wewe (Dereva). Abiria wataona jina la dereva, gari, nambari ya simu, picha na taarifa ya eneo la ki-jiografia. Abiria pia huona taarifa ya dereva binafsi katika stakabadhi..
- Kulingana na eneo la dereva, taarifa binafsi inaweza kutolewa kwa ofisi za matawi ya Bolt, wawakilishi, washirika, mawakala nk. uhifadhi wa taarifa ya kibinafsi utafanyika chini ya masharti sawa na yaliyowekwa katika sera hii ya faragha.
5. Usalama na upatikanaji
- Taarifa yoyote binafsi iliyokusanywa wakati wa kutoa huduma huhamishiwa na kuhifadhiwa katika vituo vya kuhifadhi taarifa vya Zone Media LTD na / au Amazon Web Services Inc, ambazo ziko katika nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya. Ni wafanyakazi walioidhinishwa tu, wa makampuni ya Bolt na washirika ndio wanapata taarifa binafsi na wanaweza kupata taarifa kwa lengo la kutatua masuala yanayohusiana na matumizi ya huduma (ikiwa ni pamoja na migogoro kuhusu huduma za usafiri).
- Kampuni ya Bolt na washirika wanaweza kufikia taarifa binafsi kwa kiasi kikubwa ili kutoa msaada kwa wateja katika nchi husika, angalia zaidi https://bolt.eu/cities/ ↗.
6. Uhifadhi wa taarifa binafsi abiria
- Huruhusiwi kuhifadhi taarifa binafsi za abiria pasipo idhini yetu. Huruhusiwi kuwasiliana na abiria yeyote au kukusanya, kurekodi, kuhifadhi, kutoa ruzuku au kutumia taarifa binafsi iliyotolewa na abiria au iliyopatikana kwako kupitia programu ya Bolt kwa sababu yoyote isipokuwa kwa ajili ya kutimiza huduma za usafiri.
- Lazima uzingatie kanuni na masharti ya uhifadhi wa taarifa binafsi za abiria kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya faragha ya Abiria (http://www.bolt.eu/legal/ ↗). Ikiwa unakiuka kanuni za uhifadhi wa taarifa binafsi za abiria, tunaweza kufunga na kuondoa akaunti yako ya udereva na kudai fidia kutoka kwako.
7. Upatikanaji, urekebishaji, uhifadhi, uondoaji wa taarifa
- Taarifa binafsi inaweza kutazamwa na kusahihishwa katika wavuti ya dereva.
- Taarifa zako binafsi zitahifadhiwa maadamu una akaunti hai ya udereva ya kazi. endapo akaunti yako itafungwa taarifa binafsi itahifadhiwa kwa kipindi cha ziada cha miaka 3.
- Taarifa muhimu kwa madhumuni ya uhasibu zitaifadhiwa kwa miaka 7.
- Katika tuhuma za makosa ya Kiutawala au ya jinai, udanganyifu au habari za uongo, taarifa itahifadhiwa kwa miaka kumi (10).
- Katika mazingira ya migogoro,taarifa itahifadhiwa mpaka madai yatakapothibitishwa au tarehe ya mwisho ya madai hayo.
- Tunajibu maombi ya kufuta na kuhamisha taarifa binafsi yaliyowasilishwa kwa njia ya barua pepe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja (1) na kutoa muda wa kufuta taarifa na kuihamisha.
8. Usuluhishi wa migogoro
- Migogoro inayohusiana na uhifadhi wa taarifa binafsi itatatuliwa kupitia msaada wa wateja(info@bolt.eu) ) au kwa kuwasiliana na Afisa wa Ulinzi wa taarifa wa Bolt (privacy@bolt.eu).
- Mamlaka ya usimamizi ipo chini ya Ulinzi wa Taarifa wa Kiestonia www.aki.ee ↗)ambao unaweza kuwasiliana kwa barua pepe info@aki.ee.