Kuangalia salio lako la sasa na mapato, nenda kwenye mapato kama inavyoonekana kutoka kwenye kurasa kuu na chagua saa inayofaa (kila siku, kila wiki au kila mwezi). Bonyeza kwenye mapato au gharama kukagua habari kwa kina.
Ikiwa huwezi kupata vipengele fulani vya salio, tafadhali kagua kama moja kati ya yatufatayo yanatumika:
- Ikiwa bei ya safari iko chini ya ukaguzi, jumla itaongezwa siku ambayo ukaguzi utakamilika. Kama safari iko chini ya ukaguzi hakutakuwa na bei ya mwisho kwenye historia ya safari pia. Kwa kawaida mapitio ukamilishwa ndani ya siku 1-3.
- Bonasi inaweza kuongezwa kwenye salio kwa kuchelewa na kuongezwa mwishoni mwa kipindi cha kufuzu
- Kwa kampeni za bonasi zinazoendeshwa kwa muda mrefu, kiwango cha bonasi kitaongezwa baada ya kutimizwa vigezo katika uchache na kusasishwa baada ya kumaliza kila safari. Jumla ya mwisho ya bonasi itapatikana tu mwisho wa kipindi cha kufuzu.
- Fidia kawaida huongezwa mwishoni mwa mzunguko wa malipo.
Tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi ikiwa una maswali yoyote kuhusu salio lako.