Ikiwa akaunti yako imesimamishwa:
- Hutaweza kwenda mtandaoni
- Sababu itakuwa inaonyeshwa kwenye App pamoja na hatua zinazohitajika, ikiwa zipo.
- Kwa kusimamishwa kwa muda, tarehe ya mwisho au muda wa kusimamishwa pia utaonyeshwa kwenye programu.
- Kama hauoni tarehe au mwisho unaohusiana na kusimamishwa , Akaunti yako imesimamishwa moja kwa moja
Fuatilia hatua zinazofanan na hali yako ili kurejesha ufikiaji wako:
- Aina yoyote ya tabia mbaya: Kusimamishwa kwa akaunti kutaanza kuondolewa moja kwa moja baada ya muda ulioonyeshwa kwenye programu au baada ya kumaliza maelekezo ya lazima. Ikiwa tarehe ya mwisho ni ndani ya mwaka mmoja, wasiliana na timu yetu ya Msaada ndani ya miezi 6 ili kuomba kufunguliwa
- Hati zilizokosekana au zilizokwisha muda: Pakia hati halali kwenye Portal ya dereva
- Taarifa za akaunti zisizo sahihi: Jaza maelezo sahihi katika Portal ya Dereva.
- Uthibitishaji: Kamilisha mchakato wa uthibitishaji kwenye App. Ikiwa ufikiaji wa akaunti yako bado umefungwa, wasiliana na timu yetu ya Msaada ndani ya miezi 3 ili kuwasilisha rufaa.
- Muda wa mtandaoni umezidi kikomo kilichoruhusiwa:Kusimamishwa kwa akaunti kutaanza kuondolewa mara tu unapokuwa mtandaoni kwa muda unaoonekana kwenye app.
Ikiwa kuna hatua zozote zilizotajwa katika taaarifa kwenye app kuhusu kusimamishwa kwa akaunti, fuata maelekezo yaliyotolewa ili kufunguliwa.
Ikiwa unahitaji msaada, tafadhali wasiliana na timu yetu ya Msaada kupitia kwenye app.