Malipo yako huhesabiwa moja kwa moja kila wiki. Mzunguko wa malipo huanzia Jumatatu (00:00) hadi Jumapili ifuatayo (23:59). Ikiwa unastahili kupokea malipo, tutatuma pesa hizo katika nusu ya kwanza ya juma linalofuata.
Tutatuma malipo yako kwa akaunti ya benki au mtandao wa simu uliounganishwa na akaunti yako ya dereva. Kulingana na muda wa benki yako kuchakata malipo, inaweza kuchukua siku 1-2 za kazi kwa muamala kukamilika na malipo kupokelewa.
Ili kuona salio lako na kiasi cha malipo, nenda kwenye Mapato kama yanavyo onekana kwenye kurasa kuu ndani ya programu.