Ikiwa unataka kufuta akaunti yako, fuata hatua hizi:
- Bofya kwenye mistari mitatu ya mlalo kwenye kona ya juu kushoto ya skrini.
- Bofya badili wasifu
- Tembeza hadi chini na ubofye Futa akaunti yangu
- Chagua sababu na ubofye Futa akaunti
Inawezekana tu kufuta akaunti yako wakati malipo yoyote ambayo bado hayajalipwa yamelipwa.
Ikiwa huwezi kufuta akaunti yako, tafadhali wasiliana na timu yetu ya Usaidizi.
Akaunti yako ikishafutwa haitawezekana kurejesha maelezo yoyote yaliyo unganishwa nayo, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kadi yako ya benki, ofa zozote na Salio la Bolt.
Tafadhali kumbuka kuwa ukifuta akaunti yako, akaunti yako ya Bolt Food pia itafutwa.
Ingawa taarifa yako itafutwa, bado tunahifadhi maelezo kama vile ankara na maelezo ya malipo ili kutii sheria kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha.
Kumbuka: Kipengele hiki bado hakijatolewa kikamilifu. Ikiwa huna chaguo la kufuta akaunti yako katika programu, tafadhali omba kufutiwa akaunti kwa kuwasiliana na timu yetu ya Usaidizi.