Bolt huchakata baadhi ya taarifa zako binafsi. Unaposakinisha na kujisajili katika programu ya Bolt, unakubaliana na Sheria na Masharti yetu na kutoa idhini yako kwa ajili ya kukusanya na kuchakata taarifa zako.
Taarifa yako binafsi itahifadhiwa mradi tu uwe na akaunti inayotumika. Ili kuomba uhamisho wa taarifa yako binafsi, tafadhali wasilina na timu yetu ya usaidizi kupitia programu.
Ili kufuta taarifa yako, tafadhali tuma ombi ili akaunti yako ifutwe kupitia ujumbe wa ndani ya programu. Baadaye, taarifa yako binafsi itafutwa kutoka kwenye kumbukumbu, isipokuwa kama taarifa hiyo inahitajika kwa uhasibu, utatuzi wa migogoro, au madhumuni ya kuzuia ulaghai. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea Sera ya Faragha.