Abiria anapaswa kufidia gharama ya kusafisha/uharibifu aliofanya ndani ya gari.
Bolt itarejesha gharama za usafi kutoka kwa abiria na kufidia kwa dereva na Bolt inaweza kulipa fidia yenyewe kwa baadhi ya kesi.
Ili kuripoti kesi kama hizo, tafadhali tuma viambatanishi vifuatavyo:
- Angalau picha tatu za uharibifu uliofanyika (tizama vidokezo chini)
- Taarifa kuhusu safari (jina la abiria, mahali ulipomchukua na kumshushwa, tarehe na saa vitasaidia)
- Ripoti uharibifu mara moja kabla ya hujaanza safari nyingine (ripoti inayotumwa baada ya kuanza safari nyingine inaweza isifanyiwe kazi)
- Maelezo kwa kifupi kuhusu tukio lilivyotokea
Pai tunaweza tukakuomba utoe risiti ya usafi/uharibifu ili kuthibitisha kuwa gari limesafishwa au limefanyiwa matengenezo.
Risiti inatakiwa kuwa na vifuatavyo:
- Jina na taarifa za kampuni husika ya kusafisha magari
- Huduma iliyotolewa (mfano, usafi wa gari) na bei ya huduma hiyo
Vidokezo vya picha:
Chunguza gari lako baada ya safari kumalizika kuona kama kuna uchafu au uharibifu uliofanywa na abiria. Kumbuka vidokezo vifuatavyo:
- Chukua picha kwa karibu kutoka kona tofauti tofauti kisha chukua picha kwa mbali ili tuweze kuona kiasi cha uchafu/uharibifu uliofanyika
- Picha zinazochukuliwa lazima ziwe na muda na tarehe ya tukio
- Washa taa za ndani ya gari au tumia mwanga wa tochi kuhakikisha picha zinaonekana vizuri
Kumbuka:
- Tutakubali ombi moja tu la fidia ya usafi/uharibifu ambalo halijafuata taratibu kama zilivyoelezwa hapo juu. Baada ya hapo ombi la fidia ya usafi au uharibifu ambalo halitafuata ratatibu zetu litakataliwa.
- Gharama za fidia zitawekwa katika kikomo fulani kulingana na mji husika
- Matukio yanatakiwa kuripotiwa mara moja. Ripoti itakayotumwa baada ya kufanya safari zaidi na gari iliyochafuliwa/ kuharibiwa inaweza isifanyiwe kazi.
Wasiliana na timu yetu ya huduma kwa wateja na taarifa zote kama zilivyoelezwa hapo juu kupitia App.