Tunatafuta madereva wenye magari ili wajiunge na kuendesha na Bolt. Ili kuendesha na Bolt Tanzania, tafadhali hakikisha umefikisha mahitaji kama yalivyo orodheshwa hapa chini:
Mahitaji ya chombo cha usafiri
- Modeli ya gari lazima iwe ya mwaka 1998 au mpya zaidi
- Modeli ya pikipiki lazima iwe ya mwaka 2005 au mpya zaidi
- Modeli ya Bajaji lazima iwe ya mwaka 2005 au mpya zaidi.
Nyaraka zinazohitajika
- Picha
- Pasipoti au kadi ya kitambulisho
- Leseni ya Udereva
- Kadi ya Usajili wa Chombo cha Usafiri
- Bima ya chombo cha usafiri
- Hati ya tabia njema (inayopatikana wizara ya mambo ya ndani).
Nyaraka za ziada kwa ajili ya Bajaji, Boda na Gari
- Leseni ya Latra
- Leseni ya TRA.
Kamilisha hatua zifuatazo kujiunga na kuendesha nasi:
- Hatua ya kwanza: Jiunge mtandaoni ili kuanza mchakato wa kujisaliji
- Hatua ya pili: Pakia nyaraka na taarifa zako
- Hatua ya tatu: Hudhuria mafunzo na kisha akaunti yako itasajiliwa.
Kumbuka: Vyombo vya usafiri vinathibitishwa ndani ya masaa 2-6 baada ya kukusanywa.