Ikiwa unahitaji kulipa kamisheni ya Bolt, tafadhali angalia maelezo yafuatayo:
- Je unalipaje kamisheni?
- Nini cha kuthibitisha kabla ya klumpa kamisheni?
- Inachukua muda gani mchakato wa malipo kukamilika?
Je, unalipaje kamisheni?
Ikiwa una salio hasi, unaweza kulipa kamisheni ya Bolt kwa kuhamisha pesa kupitia programu kwenye simu.
Jinsi ya kufanya hivyo:
- Nenda kwenye sehemu ya Mapato na kisha bonyeza kitufe cha Lipa kwa Bolt
- Chagua chaguo la kulipa (mtandao wa simu unaotumia)
- Ingiza nambari ya simu unayotaka kulipa nayo
- Fuata maagizo katika programu ili kukamilisha malipo
- Subiri kupokea uthibitisho wako wa malipo kabla ya kufunga au kusogea mbali na lango la malipo.
Nini cha kuthibitisha kabla ya kulipa kamisheni?
Kabla ya kuthibitisha malipo, hakikisha:
- Maelezo ya akaunti yako ya simu uliyoingiza ni sahihi.
- Unatumia Vodacom Mpesa au Airtel Money. Kwani programu yetu ya malipo haiendani na mitandao mingine.
- Una fadha za kutosha kulipa pesa zote unazodaiwa. Huwezi kubadilisha jumla ya fedha inayotakiwa kulipwa.
Inachukua muda gani mchakato wa malipo kukamilika?
Mara tu malipo yakithibitishwa, inaweza kuchukua hadi masaa 24 kwa kiasi hicho kuonekana katika salio lako.