Ada ya kuhifadhi ni malipo ya ziada kwa kila safari anayoomba mteja. Malipo hayo yanasaidia katika utoaji wa msaada pamoja na vipengele vipya vya usalama na ulizi ambapo tutahakikisha vinazingatiwa zaidi katika mfumo wa huduma yetu.
Malipo haya yatajumuishwa moja kwa moja katika nauli ya wateja wote kwa malipo ya fedha taslimu na kadi pia.
- Safari za fedha taslimu: Ada ya kuhifadhi 3.6% itaongezwa katika nauli ya mteja, kwa sababu malipo ni ya fedha taslimu na unapokea pesa hiyo, tutatoa jumla ya kiasi hiki kwenye mapato yako ya wiki.
- Safari za kadi: Ada ya kuhifadhi 3.6% itajiongeza moja kwa moja katika nauli ya mteja na Bolt itaikusanya hapo hapo.
Kiwango hiki kitaonekana vilevile katika mapato yako ya wiki, ada ya kuhifadhi kwa safari za fedha taslimu na malipo ya kadi itahesabiwa na tutaikusanya hapohapo.
Je hili litaathiri kipato changu?
Hapana ada ya kuhifadhi haitaathiri kamisheni au ada yoyote ya bei katika mapato yako.