Unaweza kuunganisha mfumo wa gharama wa kampuni yako kwenye wasifu wako wa kazini ili stakabadhi za safari za Bolt zitumwe moja kwa moja kwa mtoaji gharama. Inawezekana ukatumia Zoho Expense, Expensify, Rydoo na SAP Concur. Tafadhali angalia ni watoa huduma gani wanaopatikana katika nchi yako.
Jinsi ya kuunganisha mtoa huduma wa gharama kwenye wasifu wako wa kazini:
- Nenda kwenye kichupo cha Safari za kazini katika menyu
- Fungua chaguo la Ongeza mtoaji gharama
- Fuata maagizo kwenye tovuti ya jukwaa ili kukamilisha mchakato.
Vinginevyo, unaweza kuifanya kwenye tovuti ya anaetoa huduma ya kugharamia
Tafadhali fahamu kuwa ukibadilisha barua pepe yako kwa ajili ya risiti, utahitaji kuunganisha tena mtoaji huduma za gharama.
Ili kumuondoa mtoaji huduma wa gharama kwenye wasifu wako wa kazini, nenda kwenye Safari za kazini kutoka kwenye programu, chagua mtoa huduma wa gharama na ubofye kitufe cha kufuta
Ikiwa unatatizo lolote, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wa gharama.