Siwezi kuingia katika akaunti yangu ya udereva

Kama huwezi kuingia katika akaunti yako ya udereva, tafadhali hakikisha:

  • Jina la mtumiaji na neno lako la siri ni sahihi
  • Hakikisha una fursa ya matumizi kwa namba ya simu iloonganishwa na akaunti yako ya dereva, ili uweze kupokea neno la siri la wakati mmoja kupitia SMS (ikiwa inahitajika katika kuingia)
  • Akaunti yako imeidhinishwa. Akaunti yako ikiwa imeidhinishwa, utapokea maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako katika barua pepe yako.

Nambari ya uthibitisho ya mara moja inatumwa kwa nambari ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya dereva. Ikiwa namba hii ya simu ipo hewani lakini haukupokea nambari ya uthibitishaji, tafadhali jaribu:

  • Kuanzisha tena simu yako
  • Kuomba tena kutumiwa nambari ya uthibitishaji. Inachukua hadi sekunde 60 kwa nambari kukufikia.

Kama unahitaji msaada wowote, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi kupitia barua pepe help@bolt.eu.

Request in seconds, ride in minutes.

Available for iOS and Android devices.
Request in seconds, ride in minutes.