Ilani ya Ufaragha kwa Abiria na Wasafirishaji

Ilani hii ya ufaragha inakujulisha jinsi tunavyoahidi kutunza data yako ya kibinafsi. Ilani hii inakuambia mambo kama vile taarifa tunayotumia kukupa kifurushi chetu cha huduma za usafirishaji, jinsi tunavyotumia taarifa yako kukuweka salama, na chaguzi na udhibiti unaoweza kupata. Ilani hii pia inakuambia kuhusu haki zako za faragha na jinsi sheria za ulinzi wa data zinavyolinda kila mtu.

Bolt Operations OÜ ndiyo Mdhibiti wa data yako ya kibinafsi isipokuwa ikielezwa vinginevyo hapa chini.

Anwani yetu ya posta ni : Vana-Lõuna 15 Tallinn 10134 Estonia

Tumeteua Afisa wa Ulinzi wa Data, na unaweza kuwasiliana naye kwenye privacy@bolt.eu au kupitia anwani yetu yoyote ya posta inayopatikana kwenye city pages. Tafadhali andika kwenye bahasha ‘Afisa wa Ulinzi wa Data’.

Neno "sisi" linamaanisha mmiliki wa programu ya Bolt, Bolt Operations OÜ, kampuni ya kibinafsi, iliyoanzishwa katika Jamhuri ya Estonia. Neno “wewe” au“-ako” linamaanisha abiria au msafrishaji anayeomba, anayekodisha na/au anayepokea huduma ya usafirishaji kupitia akaunti yake ya programu ya Bolt.

1. Data ya kibinafsi ambayo tunashughulikia

Tunashughulikia tu taarifa ambayo tunahitaji, ili tuweze kukupa huduma bora kwenye soko letu la usafirishaji.

 • Maelezo ya uwasiliano: kama vile jina, nambari ya simu na anwani ya barua pepe. Tunaweza kuhitaji mambo zaidi, kama anwani yako ya nyumbani, katika huduma zetu nyingine.
 • Taarifa fupi kukuhusu: kama vile picha yako ya umbopande, anwani zilizohifadhiwa, lugha na mawasiliano unayopendelea. Tunaweza kuhitaji mambo zaidi, kama maelezo ya leseni yako ya udereva, katika huduma zetu nyingine.
 • Eneo la Kijiolojia: kama vile mahali uliko unapohitaji huduma ya usafiri, au eneo la pikipiki zilizo karibu nawe, wakati, mwendo wa safari na unakoenda.
 • Taarifa ya malipo kama kiasi kilichotozwa na kadi ya malipo iliyotumiwa.
 • Rekodi za mawasiliano kama vile unapozungumza katika programu yetu, au unapozungumza na mawakala wetu wa huduma kwa wateja.
 • Kudhibitiwa kwa data za utambulisho wa kifaa, kama vile anwani ya IP, ambayo programu ya Bolt imewekwa
 • Data kuhusu kutumia huduma za usafirishaji: mambo kama vile data kuhusu hali ya safari, nyakati na data kuhusu mwenendo wako kama ilivyotathminiwa na madereva.
 • Data zinazohusiana na mawasiliano kupitia ujumbe wa papo hapo wa moja kwa moja kwenye programu ya Bolt (chaguo la "Ongea na Dereva"): tarehe na wakati wa mawasiliano na maudhui.

2. Sababu ya kushughulikia

Tunashughulikia data yako ya kibinafsi ili tuweze kukupa mojawapo ya huduma zetu za usafirishaji au zaidi:

 • Tunakuunganisha na dereva, kukusaidia kupata pikipiki au kukodisha gari: Tunakusanya na kushughulikia data ya kibinafsi kwa sababu ya kuunganisha abiria na madereva ili uweze kuchukuliwa na kupelekwa unakoenda; au kukuonyesha mahali karibu ambako magari yetu ya kukodisha yanapatikana, kama vile magari au pikipiki zetu. Ujumbe wa papo hapo moja kwa moja kwenye programu ya Bolt unashughulikiwa ili kutoa huduma na msaada kwa wateja (ikiwemo kutatua migogoro kati ya dereva na abiria), kwa sababu za usalama na pia kuboresha bidhaa na huduma zetu, na kwa ajili ya uchambuzi.
 • Tunakufikisha mahali unakotaka kwenda: Tunawaonyesha madereva data ya eneo la kijiolojia na nambari ya simu ya abiria wakati wa kusafiri kwa ajili ya kurahisisha kuchukuliwa na kupelekwa unakoenda, na kuona safari na njia. Data hizi hukusanywa tu wakati programu ya Bolt inatumika. Ukusanyaji wa data za eneo la kijiolojia husimamishwa baada ya kufunga programu ya Bolt. Katika nchi nyingine madereva hawawezi kuona nambari za simu za abiria; dereva huona nambari tofauti kabisa ambayo inamuelekeza kwa nambari ya simu ya abiria kwa muda ikimaanisha kwamba dereva na abiria bado wanaweza kuwasiliana.
 • Tunahakikisha kwamba safari yako inakwenda sawa: Tunatumia data za eneo la kijiolojia o ili kuhakikisha kwamba unafika unakoenda na kutatua maswala ya ubora yanayohusiana na huduma zetu. Tunahitaji pia kujua mahali umechagua kuondoka kwenye chombo cha usafiri cha kukodisha ili tuweze kutoza bili sahihi, kuchaji betri tena na kutunza magari yetu.
 • Tunahakikisha kwamba programu inafaa kabisa: Tunatumia maelezo ya mawasiliano kuwajulisha abiria na wasafirishaji kuhusu habari za programu ya Bolt ili uweze kuendelea kutumia huduma zetu. Pia tunakusanya data chache kutoka kwenye kifaa unachotumia kukuunganisha na intaneti yetu, huduma za rununu na simu, na kusaidia kuweka akaunti yako salama kupitia uthibitishaji na ukaguzi.
 • Tunahakikisha kwamba safari yako ni ya haraka zaidi, ya bei rahisi na inayokufaa zaidi: Tunakusanya data kuhusu njia ambazo abiria na wasafirishaji wetu wanapitia ili kuchambua kijiolojia maeneo ambapo huduma zetu zinatolewa. Hii inatuwezesha kufanya mambo kama vile kuboresha mapendekezo kwa madereva kuhusu njia bora zaidi, na hutusaidia kuhakikisha kwamba vyombo vyetu vya usafiri vya kukodisha, kama vile pikipiki zetu, ziko katika maeneo yaliyo rahisi sana kufikiwa na wateja.
 • Tunakusanya malipo yako: Tunapata maelezo ya malipo ili tushughulikie malipo ya abiria kwa niaba ya madereva kwa ajili ya kukodisha gari. Na tunashughulikia malipo ya vyombo vyetu wenyewe vya usafiri vya kukodisha, kama vile magari yetu na pikipiki.
 • Tunadumisha na kukuza viwango: Tunakusanya data kuhusu hali za safari, saa na ukadiriaji wa abiria kutoka kwa maoni ya dereva ili kuhamasisha usalama wa mtumiaji, kukuza kufuata sheria na masharti yetu, na kuhakikisha kwamba tunatoa huduma bora na inayofurahisha kila mtu. Data ya usaidizi wa mteja na mawasiliano hukusanywa kwa ajili ya maoni, na kutatua migogoro na maswala ya ubora wa huduma.
 • Tunakufahamisha: Jina lako, nambari yako ya simu na anwani ya barua pepe zitatumika kuwasiliana nawe kwa ajili ya kukujulisha kwamba safari yako imekamilika, kukutumia hati za uthibitisho wa safari na risiti, na kukujulisha kuhusu masasisho muhimu ya huduma kama vile hali mbaya ya hewa ikizuia pikipiki zetu kukodishwa.

3. Msingi wa Kisheria

Tunaruhusiwa kutumia taarifa ya kibinafsi kwa njia zilizoelezwa hapa juu ikiwa tuna sababu inayofaa ya kufanya hivyo. Huwa tunahakikisha kwamba tuna sababu nzuri ya kutumia data yako kwa njia yoyote.

 • Data za kibinafsi hushughulikiwa ili kutoa huduma ulizoomba kupitia programu ya Bolt. Hii inamaanisha kwamba ili tukupe huduma tuliyokuahidi, na kutimiza sheria na masharti yetu, tutashughulikia data yako ya kibinafsi ili tutimize wajibu huo.
 • Katika hali nyingine huwa tunashughulikia data yako ya kibinafsi kulingana na sababu za masilahi halali. Masilahi halali yanajumuisha masilahi yetu ya kibiashara katika kutoa huduma ya ubunifu, ya kibinafsi, salama na yenye faida kwa abiria wetu na washiriki wetu, isipokuwa kama masilahi hayo ni muhimu zaidi kuliko masilahi mengine. Masilahi yetu halali pia yanajumuisha mambo kama vile kuchunguza na kugundua malipo ya ulaghai na shughuli nyingine mbaya, kudumisha usalama wa mtandao wetu na mifumo, na kushughulikia vitendo vya uhalifu vinavyoshukiwa na vilivyotendwa.

Mara kwa mara tunaweza kutegemea misingi mbadala ya kisheria ikiwa:

 • ni muhimu kuzingatia wajibu wa kisheria kama vile kushughulikia data wakati sheria inahitaji, pamoja na, kwa mfano, ikiwa kuna ombi halali la kisheria la kufichua taarifa za kibinafsi kwa mtu asiyehusika moja kwa moja kama vile Mahakama au mamlaka ya udhibiti;
 • kulinda maslahi yako muhimu, au ya watu wengine, kwa mfano wakati wa dharura au kukiwa na tishio kwa maisha; au
 • umetupea idhini wazi ya kufanya hivyo kwa kusudi lingine maalum ambalo umejulishwa kikamilifu.

Katika nchi ambapo maslahi halili sio sababu ya kisheria ya kufanya shughuli za Bolt, kama vile nchini Nigeria, Bolt hutegemea njia mbadala halali iliyo hapa juu.

Ukiamua kwamba hutatupea taarifa za kibinafsi huenda ukatuzuia kufanya mkataba na wewe, au kutuzuia kufanya jambo ambalo sheria inatarajia tufanye. Inaweza pia kumaanisha kwamba hatuwezi kuendesha shughuli kwenye akaunti yako. Kwa mfano, tunakusanya na kushughulikia data ya kibinafsi iliyowasilishwa wakati wa kusanikisha na kutumia programu ya Bolt; kukataa kushiriki data ya mahali ulipo kupitia Programu kunamaanisha kwamba hatuwezi kumuelekeza dereva kwa eneo lako ili akuchukue, wala hatuwezi kukuonyesha mojawapo wa magari yetu yaliyo karibu na wewe ili ukodishe. Hatutaweza kutimiza majukumu yetu kwako katika hali nyingine, kwa mfano, ukikataa kuthibitisha utambulisho ili kuhakikisha uadilifu wa akaunti yako, basi akaunti inaweza kusimamishwa au kufungwa ili kuzuia udanganyifu.

4. Wapokeaji

Tunashirikiana tu na washirika na mamlaka ya kuaminika. Tunashiriki tu kukiwa na sababu nzuri ya kufanya hivyo. Tunashiriki tu mambo yanayohitajika. Hatuuzi taarifa yako ya kibinafsi.

 • Data za kibinafsi za abiria zinafichuliwa tu kwa madereva waliokodisha magari wanaposafiri kwa kutumia programu ya Bolt; katika hali kama hiyo, dereva ataona jina, nambari ya simu (katika nchi nyingine nambari inafichwa) na data ya mahali abiria alipo.
 • Baada ya kutoa huduma ya usafirishaji, dereva ataendelea kuona jina na nambari ya simu (katika nchi nyingine nambari inafichwa) ya abiria kwa saa 24-48. Hii ni muhimu ili madereva waweze kusuluhisha maswala yoyote na abiria kama vile kukurudishia kitu fulani ambacho kilibaki garini. Lo!
 • Maoni yanayotolewa na abiria kuhusu ubora wa huduma ya usafirishaji hayakutambulishi. Makadirio yako ni ya faragha kati yako na Bolt .
 • Kulingana na eneo la abiria, data ya kibinafsi inaweza kufichuliwa kwa vikundi vya kampuni na washirika wa Bolt Operations OÜ (tanzu za eneo hilo, wawakilishi, washirika, mawakala nk). Vikundi vya kampuni na washirika wa Bolt Operations OÜ watashughulikia data ya kibinafsi kulingana na masharti yaliyoanzishwa katika ilani hii ya faragha. Unaweza kusoma zaidi kwenye ukurasa wako wa nchi.
 • Katika hali nyingine sheria inatulazimisha kushiriki taarifa na wapokeaji wa nje. Kwa mfano, chini ya Agizo la Mahakama au ambapo tunashirikiana na mamlaka ya usimamizi wa ulinzi wa data katika kushughulikia malalamiko au uchunguzi. Tunaweza pia kujibu maombi, kama vile maombi yanayotoka katika mashirika ya utekelezaji wa sheria, tunapoamini kwamba jibu linahitajika na sheria katika mamlaka hiyo au linaendeleza jukumu la masilahi ya umma, linaathiri watumiaji walio katika mamlaka hiyo, na linalingana na viwango vinavyotambuliwa kimataifa. Katika tukio lolote, tutahakikisha kwamba tuna msingi halali wa kushiriki taarifa, natutahakikisha kwamba tunaandika uamuzi wetu.

5. Usalama na upatikanaji

 • Data yoyote ya kibinafsi iliyokusanywa wakati wa kutoa huduma zetu huhamishwa na kuhifadhiwa katika vituo vya data vya Zone Media Ltd. na/au Amazon Web Services, Inc., ambazo ziko katika Nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Ulaya. Wafanyakazi walioidhinishwa pekee wa vikundi vya kampuni na washirika wa Bolt Operations OÜ ndio wanaoweza kupata data ya kibinafsi na wanaweza kupata data hiyo tu kwa kusudi la kutatua maswala yanayohusiana na utumiaji wa huduma (ikiwa ni pamoja na mizozo inayohusu huduma za usafirishaji).
 • Vikundi vya kampuni na washirika wa Bolt Operations OÜ wanaweza kupata data ya kibinafsi kwa kiwango kinachohitajika ili kutoa usaidizi kwa wateja katika nchi husika.
 • Kwa madhumuni yetu ya utafiti na ya kisayansi, data zote, kama data ya mahali watu walipo, hazitiwi jina kwa hivyo hauwezi kutambuliwa.

6. Haki na udhibiti wako

Tunakutaka uwe na uwezo wa kudhibiti data yako ya kibinafsi. Bolt inakupa udhibiti kupitia programu ambapo unaweza kuona taarifa yako ya kibinafsi ikiwemo data ya maelezo kukuhusu na historia ya safari. Tunatoa pia mipangilio ya ndani ya programu kama ruhusa ya kutumia habari za uuzaji, na udhibiti wa idhini ya kidakuzi kwenye tovuti yetu. Haki yako ya ufikiaji

 • Unaweza kupata data yako ya kibinafsi kupitia programu ya Bolt. Una haki ya kutuomba nakala za taarifa yako ya kibinafsi. Kuna hali ambapo hutaruhusiwa kufanya hivyo, kama vile wakati tunapaswa kusawazisha haki za watu wengine, inayomaanisha kwamba huenda usipokee taarifa zote tunazoshughulikia kila wakati.

Haki yako ya kurekebisha

 • Unaweza kupata na kusasisha data yako ya kibinafsi kupitia programu ya Bolt. Una haki ya kutuomba turekebishe taarifa unayofikiria kwamba sio sahihi. Pia una haki ya kutuomba tukamilishe taarifa unayofikiria kwamba haijakamilika.

Haki yako ya kufuta Una haki ya kutuomba tufute taarifa yako ya kibinafsi katika hali fulani. Haki yako kwa kuzuia ushughulikiaji

 • Una haki ya kutuomba tuzuie ushughulikiaji wa taarifa yako ya kibinafsi katika hali fulani. Hii inamaanisha kwamba data yako inaweza kutumika tu katika hali fulani, kama vile madai ya kisheria au kutumia haki za kisheria.

Haki yako ya kupinga ushughulikiaji

 • Huenda uwe na haki ya kupinga ushughulikiaji ikiwa tunashughulikia taarifa yako kwa ajili ya masilahi halali. Unaweza kupinga uamuzi wowote wa kiotomatiki ambao tumefanya, na kuomba kwamba mtu akague uamuzi huo.

Haki yako ya kupata na kutumia data

 • Una haki ya kuomba kwamba tuhamishe taarifa uliyotupea kutoka katika shirika moja hadi lingine, au tukupe, katika hali fulani. Hii inatumika tu katika taarifa uliyotupea.
 • Kipindi cha kuweka data inayohusu jumbe za papo hapo za moja kwa moja kwenye jumbe za programu ya Bolt ni siku 90, isipokuwa ambapo jumbe hizo ziwe zinahusiana na tukio lililoripotiwa - katika hali hiyo tutazihifadhi kwa miezi 6.

7. Kuweka

Bolt huhifadhi data ya mtumiaji kwa muda mrefu tu kama inahitajika kwa madhumuni yaliyoelezwa hapa juu. Hii inamaanisha kwamba tunahifadhi tabaka tofauti za data kwa vipindi tofauti kulingana na aina ya data, huduma ya usafirishaji inayohusiana nayo, na sababu ambazo zilitufanya tukakusanya data hiyo.

 • Data yako ya kibinafsi itahifadhiwa kwa muda wote ambao una akaunti ya abiria inayotumika. Akaunti yako ikifungwa, data ya kibinafsi itafutwa (kulingana na ratiba na sheria zetu za kuweka), isipokuwa kama data hiyo bado inahitajika kutimiza wajibu wowote wa kisheria, au kwa ajili ya uhasibu, utatuzi wa migogoro au kwa ajili ya kuzuia udanganyifu.
 • Data za kifedha zinazohusu huduma za usafirishaji zinazotolewa kwa abiria zitahifadhiwa kwa miaka mitatu baada ya safari ya mwisho. Data zinazohitajika kwa sababu nyingine za uhasibu zitahifadhiwa kwa miaka saba baada ya safari ya mwisho.
 • Ikitokea kosa la jinai linaloshukiwa, shughuli za ulaghai au habari za uwongo zikitolewa, data inaweza kuhifadhiwa mpaka miaka 10.
 • Kukiwa na mizozo kuhusu malipo, data itahifadhiwa hadi dai hilo lisuluhishwe au itakapofika tarehe ya mwisho ya madai kama hayo.
 • Data za historia ya safari na data inayohusu utumiaji wa huduma za usafirishaji zitahifadhiwa kwa miaka mitatu, baada ya hapo data hiyo haitatiwa jina.

Tafadhali jua kwamba kuiondoa programu ya Bolt kwenye kifaa chako hakusababishi data yako ya kibinafsi kufutwa. Ikiwa programu ya Bolt haijatumika kwa miaka mitatu, tutawasiliana nawe na kukuomba uthibitishe ikiwa ungependa kuweka akaunti yako ili uitumie kwa siku zijazo. Tusipopokea jibu kwa wakati unaofaa, akaunti itafungwa na data ya kibinafsi itafutwa isipokuwa kama data hiyo inahitajika kwa sababu yoyote iliyotajwa hapo awali kwenye ilani hii ya ufaragha.

8. Utangazaji wa moja kwa moja

 • Tunaweza kutuma ujumbe wa utangazaji wa moja kwa moja kwenye anwani yako ya barua-pepe na/au nambari ya simu ukituruhusu ya kufanya hivyo, au bila ruhusa yako mahususi. Tunaweza kutuma ujumbe wa utangazaji kwa kuzingatia mtu binasfi moja kwa moja kwa kutumia taarifa kuhusu unavyotumia huduma za Bolt ,kama vile unatumia programu ya Bolt mara ngapi, na upendeleo wako wa usafiri.
 • Ikiwa hutaki tena kupokea ujumbe wa utangazaji wa moja kwa moja, tafadhali bofya kiungo cha "Futa usajili" kilicho kwenye kijachini cha mojawapo wa barua pepe zetu, au ujiondoe kwenye sehemu ya umbopande wa programu ya Bolt. Rahisi.

9. Kufanya uamuzi kiotomatiki

Tunatumia uamuzi wa kiotomatiki katika kutoa maonyo na kusimamisha huduma ya safari. Kutumia uamuzi wa kiotomatiki hakusababishi makosa mengi, kunafaa zaidi na ni salama kuliko kutumia wafanyakazi wetu. Data inayohusu utumiaji wako wa huduma za usafirishaji (data kuhusu hali ya safari ikiwemo kufuta na kutokuwepo na data kuhusu mwenendo wako kulingana na madereva) inachukuliwa wakati wa kutathmini hitaji la onyo au kusimamishwa. Unaweza kusoma mambo mengi kuhusu uamuzi wa kiotomatiki hapa. Kusimamishwa kwa huduma ya usafirishaji kutaendelea kwa miezi 6, baada ya hapo utaweza kurejeshewa huduma ya usafiri.

Utakuwa na haki ya kibinadamu kutathimini uamuzi huo na kupinga uamuzi huo, kutoa maoni yako na kupata maelezo kwa kuwasiliana na huduma ya usaidizi kwa wateja wetu iliyo katika programu yetu.

10. Utatuzi wa migogoro

 • Migogoro inayohusiana na kushughulikia data ya kibinafsi unatatuliwa kupitia huduma ya usaidizi kwa wateja (info@bolt.euu) katika hali ya kwanza. Una haki ya kuwasiliana na Afisa Ulinzi wa Data wa Bolt (privacy@bolt.eu).
 • Mamlaka yetu ya usimamizi ni Ukaguzi wa Ulinzi wa Data wa Kiestoniawww.aki.ee).

11. Kufanya ilani hii iwe nzuri

Tunatarajia kwamba umeweza kuelewa ilani hii ya faragha kwa rahisi.

Sheria za ulinzi wa data ni muhimu. Zinaimarisha sheria na kuboresha haki zako za taarifa. Huenda uone kwamba baadhi ya sheria hizi ni ngumu kuelewa, lakini nyingi zinahusu mambo ya kawaida. Tunazingatia majukumu yetu kuhusu data yako kwa umakini. Bolt itaendelea kufanya mabadiliko kwenye ilani hii ya faragha kama sehemu ya ahadi yetu ya kulinda faragha yako na kukupa uwazi zaidi.

Taarifa zaidi zinapatikana katika Sheria na Masharti ya eneo husika kwa Abiria.